Baadhi ya Wanachama wa CHADEMA wakishangilia kwa furaha baada ya Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema kuachiwa kwa dhamana mahakama kuu leo jijini Arusha.
Lema ameachiwa kwa dhama ikiwa ni takribani miezi minne tangu awekwe rumande kwa kesi ya uchochezi.
Arusha. Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) Godbless Lema, ameachiwa kwa dhama leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.
Lema ameachiwa kwa dhama ikiwa ni takribani miezi minne tangu awekwe rumande kwa kesi ya uchochezi.
Polisi wa kutuliza ghasia walijaa mahakamani hapo wakiwafukuza wafuasi wa Lema waliojaa katika viwanja vya mahakama hiyo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe walikuwepo mahakamani hapo leo.
Post a Comment