hot stuff

MAHAKAMA YAMPA WEMA SEPUTU DHAMANA

Leo kwenye Mahakama ya hakimu mkazi kisutu Dar es salaam alifikishwa Mwigizaji Wema Sepetu ambaye kuanzia wiki iliyopita alikua akishikiliwa na jeshi la Polisi kwenye sakata la dawa za kulevya.

Mahakamani Kisutu leo imekubali kutoa dhamana ya mwigizaji huyo ambapo imehusu Wadhamini wawili na milioni 5 ambapo pia tarehe 22 mwezi huu anarudi tena Mahakamani kusikiliza majibu ya Mkemia Mkuu wa Serikali kujua kama ni mtumiaji wa dawa za kulevya.

Hakimu pia alimwambia Mwendesha mashtaka alete hilo jibu la Mkemia mkuu mapema iwezekanavyo, endelea kukaa
karibu na bongohot.com
Post a Comment

Post a Comment