Kuna wakati mwingine kwenye maisha tunajitahidi kujikinga zaidi ya harufu mbaya ya miili yetu. Iwe wakati unaenda gym au katika vikao mbalimbali deodorant hutufanya tujiskie huru na wenye furaha kwani huzuia harufu mbaya itokanayo na jasho.
Kuchagua deodorant sahihi ni sawa na jinsi ya kuchagua nguo nzuri na bora tunavyofanya kila siku. Unahitaji kuchagua deodorant sio tu ambayo itakupa kinga ya muda mrefu pia ni lazima isikuletee madhara yeyote.
Jua tofauti kati ya Antiperspirants na Deodorants
Licha ya kuwa watu wengi wamekuwa wakiyachanganya maneno haya, lakini ni vitu viwili tofauti. Antiperspirants inafanya kazi kwa kuzuia usitokwe na jasho kwa kuathiri tezi za jasho (sweat gland). Deodorants zinaruhusu jasho kutoka lakini huzuia jasho. Deodorant hufanikisha kazi yake kwa kuua bacteria ambao wanasababisha harufu kwenye jasho.
Kama tukisimamia katika point hii utakuta deodorants ni bora kuliko antiperspirants kwakua inatumia njia bora ya asili. Kwa upande mwingine hakuna mtu anayefurahia kutoa harufu mbaya, isiyovutia na hata sisi wengine hatupendi kutokwa na jasho.
Tatizo linakuja kwamba bidhaa nyingi zinazofanya kazi hizi huwa zina kiambato cha Aluminium. Aluminium ni neurotoxin. Sisemi kuwa deodorant zote zina aluminium, hapana zipo ambazo hazina kiambato hicho.
Hatari ya kutumia deodorant au antiperspirant yenye ALUMINIUM
Deodorants au Antiperspirants yenye Aluminium inaweza kukusababishia madhara ya kiafya. Madhara yanayoweza kutokea ni kama yafuatayo:-
• Kansa ya matiti
• Ugonjwa wa Alzheimer (Alzheimer’s Disease)
• Magonjwa ya mifupa (Bone Disorders)
• Matatizo ya Figo (Kidney Problems)
Unaweza kupata deodorants/antiperspirants ambayo haina aluminium (Aluminum-free deodorants) ambayo imechanganywa na essential oils na viambato vingine asilia. Lakini pia deodorant au antiperspirants ambazo hazina Aluminium zingine pia huwa na triclosan na propylene glycol. Triclosan huharibu tezi ya jasho vibaya zaidi ya propylene glycol
USHAURI WANGU
Utafiti wa kisayansi umeonyesha kuwa baadhi ya viambato nilivyoviainisha hapo juu vilivyomo kwenye deodorants na antiperspirants ni hatari kwa ngozi na afya yako kiujumla. Madhara ya antiperspirants ni makubwa zaidi ya deodorants ambazo zina aluminium kwa antiperspirant huzuia jasho kutoka kwa kuathiri tezi za jasho na kusababisha matatizo kama aleji (allergy) na Dermatitis.
Tezi za jasho huondoa taka mwili kutoka katika miili yetu, sasa kama taka mwili hizi hazitolewi basi ni hatari kwa afya zetu. Kabla haujanunua deodorant au antiperspirant yako hakikisha haina kiambo hatari nilichokitaja hapo juu.
Your Health, My Concern
NA
FORD A. CHISANZA
Scientist/Researcher/Pharmacist
Location: Off Mandela Road, Mabibo – External,
P.o.Box: 77150, Dar Es Salaam, Tanzania.
Mobile:+255 652466430/+255 684363584
Email: fordchisanza@gmail.com