MIILI ya watu takriban 51 wasiojulikana, waliouwawa kwenye mapambano baina ya askari wa usalama na wapiganaji wanaotaka kujitenga na walio watiifu kwa mfalme wao, imezikwa katika Jimbo la Kasese, magharibi mwa nchi ya Uganda.
Imeelezwa kuwa hakuna mtu aliyejitokeza kudai maiti hizo na inasemekana baadhi ya miili hiyo iliteketea na haikuweza kutambulika.
Watu zaidi ya 80 waliuwawa, katika ghasia za wiki iliyopita, wengi wao wakiwa walinzi wa mfalme.
Mashirika ya kutetea haki za kibinaadamu, yamewashutumu askari wa usalama kwa kutumia nguvu kubwa wakati wa tukio hilo.
Mfalme wa jadi wa Kasese, Charles Mumbere, ameshtakiwa kutokana na mauaji hayo.