international gossip

Tuzo ya MTV EMA aliyoshinda Wizkid ilitolewa kimakosa, anapewa Alikiba

MTV Europe music Awards 2016 ilifanyika weekend iliyopita ambapo Mtanzania mwimbaji staa wa bongofleva Alikiba alikua akiwania tuzo ya BEST AFRICAN ACT ambayo ilitangazwa siku ya tukio mshindi ni Mnigeria Wizkid.

Pamoja na kwamba Wizkid alitangazwa mshindi, mtandaoni ilikua inaonyesha
Alikiba ndio anaongoza kwa kupigiwa kura na hapo watu wakaanza kuuliza kwa nguvu imekuaje? hata hivyo kulionekana mabadiliko baadae kwa rekodi hizo kutoonekana mtandaoni baada ya muda kupita.

Taarifa za uhakika kutoka kwenye Management ya Alikiba Exclusive kwa bongohotz.Com ni kwamba wametumiwa taarifa na MTV EMA kwamba kuna kosa lilitokea lakini wamerekebisha na kumfikishia taarifa Wizkid kwamba tuzo haikuwa yake hivyo itachukuliwa na kupewa Alikiba .

Inaonekana Wizkid amefikiwa na taarifa na tayari post yake ya ushindi wa tuzo hiyo ameifuta kwenye mtandao wake, endelea kukaa karibu na bongohotz.com ili kila kinachonifikia nikufikishie,
Post a Comment

Post a Comment