Serikali imetoa agizo la kusitishwa kwa michakato ya kubadilisha umiliki wa klabu za Simba na Yanga na kutaka klabu hizo kubakia kwa wanachama.
Katibu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Mohammed Kiganja alisema michakato hiyo ya ubadilishaji wa mifumo ya kuziendesha timu hizo inahatarisha usalama na kuchochea vurugu michezoni.
"Sisi hatuwezi kuvumilia kuona haya ambayo yanachochea uvunjifu wa sheria, ambayo yanafanyika. Tungependa kuona taratibu za kisheria zinafuatwa na kutekelezwa.
"Baraza linaagiza mabadiliko haya yanayotaka kufanyika kwenye klabu za Simba na Yanga, yasitishwe mpaka pale zitakapofanya mabadiliko ya katiba zao," alisema Kiganja.
Alisema yako mambo mengi ambayo yanaashiria kuwa michakato hiyo haifuati taratibu zinazotakiwa.
Post a Comment