matukio

KIJANA SAID ALLY ALIYE TOBOLEWA MACHO APEWA MTAJI WA SH MILION 10

Serikali ya mkoa wa Dar es Salaam imesema itampatia Sh10 milioni Said Ally aliyevamiwa na kutobolewa macho kama mtaji katika biashara atakayoinzisha na kuisimamia.

Ahadi hiyo ilitolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati akizungumza na wanahabari na kutoa taarifa ya uchunguzi wa Ally aliyekuwa akifanyiwa vipimo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Ally alimshukuru mkuu wa mkoa huyo na Serikali kwa ujumla kwa jitihada zake za kumsaidia.

"Naomba wananchi wengine watakaoguswa na Ally wamsaidie na tutatoa utaratibu maalumu namna ambavyo watu wataweza kumchangia," alisema Makonda.
Post a Comment

Post a Comment