Dar es Salaam. Shilingi 1.4 bilioni zimekusanywa katika harambee iliyoandaliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ili kusaidia waliopata maafa ya tetemeko la ardhi mkoani Kagera Jumamosi iliyopita.
Kiasi hicho ni fedha taslimu na ahadi ambazo zimetolewa na wafanyabiashara na mabalozi wanaoziwakilisha nchi mbalimbali nchini.
Miongoni mwa wafanyabishara hao ni Kampuni za GBP, Oilcom na Moil ambazo kwa pamoja zimeahidi kukarabati shule za sekondari za Ihungo na Nyakato ambazo tayari zimefungwa.
Baadhi ya mabalozi na wafanyabiashara wameahidi kutoa fedha taslimu, mabati, saruji, vyakula na nguo.
Post a Comment