kenya

UNESCO yasaidia wanahabari nchini Kenya




Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, limesaidia wanahabari 75 nchini Kenya kushiriki mikutano iliyojadili kuhusu haki na usalama wa wanahabari.

Mikutano hiyo mitatu ilifanyika katika kaunti za Machakos, Mombasa na Nakuru, ikilenga kuwahamasisha wanahabari kuhusu haki zao, na haja ya kuwa na uelewa kuhusu usalama wao kazini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na UNESCO, katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kumeongezeka visa vya vitisho na mashambulizi dhidi ya wanahabari nchini Kenya, ambavyo vimevuruga uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kupata taarifa.

Ripoti ya utafiti mpya ulioratibiwa na UNESCO imeonesha kuwa zaidi ya wanahabari 60 walishambuliwa au kutishiwa kazini nchini Kenya mwaka jana, saba miongoni mwao wakiwa wanawake.


Post a Comment

Post a Comment