kenya

Ukimwi tishio kwa wanafunzi nchini Kenya



Serikali ya Kenya imesema kuwa karibu vijana 180,000 waliopo shule wamepata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini humo.

Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu, Margaret Mwirigi, amesema kati ya wanafunzi hao 75,000 hawapati huduma ya dawa za kufubaza makali ya virusi vya Ukimwi.

Afisa wa Baraza la Taifa la Kudhibiti Ukimwi Kenya (NACC), Celestine Mugambi, amesema vijana 14 hufa kila siku kwa matatizo ya kiafya yanayotokana na Ukimwi na 98 huambukizwa.

Akiongea katika mkutano wa mwaka wa wakuu wa shule za msingi Kenya, Bi. Mwiriga amesema kuwa hadi wanapomaliza mkutano huo wanafunzi vijana wapatoa 500 watakuwa wamekufa kwa Ukimwi.



Post a Comment

Post a Comment