Breaking news

UKAWA WAAIRISHA MAANDAMANO KWA MWEZI MMOJA

Viongozi wa upinzani, akiwemo Edward Lowassa wa Chadema, wametangaza hatua hiyo kwenye kikao na wanahabari Dar es Salaam.

Wamesema wameahirisha maandamano hayo kwa kipindi cha mwezi mmoja baada ya kusikia ombi la viongozi wa kidini na wadau wengine waliowaomba kukumbatia na kuyapa muda mazungumzo.

Mwenyekiti wa Chadema freeman aikael mbowe akitangaza kuairisha maandamano hayo adi mwezi ujao 


Viongozi wa chama hicho walikuwa wameitisha maandamano na mikutano ya kisiasa Septemba Mosi kupinga walichosema kuwa ni ukandamizaji unaoendelezwa na serikali.

Baada ya mkutano wa kikao cha Kamati Kuu ya chama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mwishoni mwa Julai, viongozi walisema: "Yapo Matukio ambayo yamekua yakifanywa na kukandamiza demokrasia na misingi ikipuuzwa na kudharauliwa."
Post a Comment

Post a Comment