Mkuu mpya wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo
Uteuzi wa Gambo unakuja takriban miezi miwili baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha mwisho mwa Juni mwaka huu.
Dar es Salaam. Rais John Pombe Magufuli amemteua Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuanzia leo Alhamisi baada ya kutengua uteuzi wa Felix Ntibenda katika mwendelezo wa mabadiliko madogo ya kuimarisha afu ya utawala wake.
Uteuzi wa Gambo unakuja takriban miezi miwili baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha mwisho mwa Juni mwaka huu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Ntibenda anahamishiwa katika ofisi yake kwa ajili ya kupangiwa majukumu mengine.
Gambo ataapishwa kesho Ijumaa saa 3 asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Post a Comment