Ukishangaa ya Musa utayaona ya firauni...!! Kama ulikua unashangaa sana kuona wanawake wa kizungu wakiwa nusu utupu basi usishangae kusikia na wanaume wakiwa wanatembea nusu utupu.
Bongohotz imenyaka hili tukio la mamia ya wanaume na wanawake nchini marekani,New York city katika beach inayoitwa Briyton beach. Mamia hao waliandamana wakiacha vifua vyao wazi kwa dhumuni la kutaka usawa kati ya mwanamke na mwanaume.
Madai ya kufanya hivyo ni baada ya kuwepo utamaduni wa kuvaa nusu utupu kwa wanawake tu huku wanaume wakiwa wamejifunika sehemu kubwa ya mwili.