CAG awageukia Watanzania

IN SUMMARY
Akizungumza na wawakilishi wa asasi za kiraia mjini hapa wakati wa usambazaji na ukusanyaji wa maoni na toleo maalum la CAG, Mkaguzi Mkuu wa Nje katika ofisi hiyo, Martin Madalo amesema kwa kufanya hivyo watawezeshausimamizi mzuri wa mali za umma.

Dodoma. Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), amewataka Watanzania kutoa taarifa katika ofisi hizo wanapoona kuna miradi iliyotekelezwa chini ya viwango au hewa ili iweze kufanyiwa ukaguzi.

Akizungumza na wawakilishi wa asasi za kiraia mjini hapa wakati wa usambazaji na ukusanyaji wa maoni na toleo maalum la CAG, Mkaguzi Mkuu wa Nje katika ofisi hiyo, Martin Madalo amesema kwa kufanya hivyo watawezeshausimamizi mzuri wa mali za umma.

Miradi hii ya maendeleo ni yetu sote na inatekelezwa huko katika maeneo yetu. Ukaguzi shirikishi unaongeza dhana ya uwajibikaji, tutoe taarifa katika ofisi ya mkaguzi au kwa viongozi wetu mahali kama kuna miradi inayotekelezwa ikiwa chini ya viwango au miradi hewa,”amesema Madalo ambaye alimwakilisha CAG.

CAG amewahakikishia Watanzania kuwa wakaguzi wako makini na wanafanya kazi zao kulingana na maadili ya utumishi wa umma na maadili ya taaluma ya ukaguzi.

Pia wadau wengi wamekuwa wakiuliza kama ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ina uhuru katika kutekeleza majukumu yake. Ofisi yangu ina uhuru wa kufanya kazi, hilo husaidia kuwezesha kukamilisha shughuli zote za kiukaguzi kwa wakati,”amesema.

Naye Mratibu wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Dodoma, Edward Mbogo amesema ripoti za CAG zimekuwa zikiwasaidia Watanzania kuongeza uelewa juu ya uwajibikaji na utawala bora.

“Watanzania wakielewa wanaweza sasa kuhoji juu ya matumizi na mapato ya fedha mbalimbali katika halmashauri zao, mitaa yao na hivyo kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa mali za umma,” amesema Mbogo.

SHARE THIS STORY

Post a Comment

Post a Comment