gossip
WOLPER ATOA MACHOZI AKIELEZEA JINSI MKONGO ALIVYOMREKODI PICHA ZA UTUPU ILI ASIMUACHE
0
Comments
![]() |
WOLPER NA MKONGO |
Msanii wa filamu Jacqueline Wolper amefunguka na kuzungumzia sababu ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake ambaye alimvalisha pete ya uchumba pamoja na kwenda kwao kwa ajili ya maandalizi ya kumtolea mahari ili amuoe.
Muigizaji huyo ambaye amekiri kutoka kimapenzi na Harmonize wa WCB, amekiambia kipindi cha Take One cha Clouds TV kuwa, Mkongo huyo ambaye alimvalisha pete ya uchumba, alikuwa ana mke pamoja na mtoto na pia alimfanyia kitendo cha kinyama cha kumrekodi picha za uchi ili asimuche.
“Mimemvumilia kumkuta na picha zangu za uchi, video zangu za uchi,” alisema Wopler huku akilia.
“Nikiongelea nimezionaje nitakuwa namvunjia heshima, kwa sababu kuna kitu kibaya alikifanya. Kuna matatizo ambayo yalitokea nikawa namkwepa, niligundua ana matatizo mengi nikawa namkwepa, nilikuwa na stress nikawa nalewa sana, nalewa mpaka nazima. Sasa siku ambayo nimelewa sana mpaka nimezima akaambiwa nilipo, nilikuwa nipo mimi, dada yangu mmoja pamoja na mdogo wangu mmoja nimelewa chakari, nimechanyikiwa siyo mimi. So kilichotokea akaja akanichukua, akanipeleka nyumbani kwake, akanivua nguo zote, nilikaa kwenye kitanda chake, nipo uchi wa mnyama, yaani sijui chochote kinachofanyika, akarekodi video na kunipiga picha,” aliongeza Wolper.
Muigizaji huyo amesema baada ya kugundua kuwa mpenzi wake huyo alimpiga picha za uchi, alimuomba azifute lakini akawa anamtishia kuzisambaza kama akimuacha.
![]() |
Harmonize na Wopler ndani ya mahaba |
Pia Wolper amedai alipelekwa Afrika Kusini ili akasome lakini akaishia kudanganywa na kukaa Afrika Kusini kwa miezi mitatu bila chochote na kuamua kurudi zake Dar es salaam.
Jiunge na BONGOHOTZ.COM sasa
Usipitwe!! kupitia FACEBOOK, TWITTER na INSTAGRAM kupata habari ndani ya sekunde kila inapotufikia..!! Usiache ku download application play store BOFYA HAPA KU DOWNLOAD....... LIKE PAGE YA BONGOHOTZ KWENYE FACEBOOKLIKE PAGE