did you know?

Waliofukuzwa Chuo Kikuu cha Dodoma waigeukia hii kazi

Moja ya story kubwa may 30 2016 kwenye gazeti la Mtanzania yenye kichwa cha habari ‘Waliofukuzwa UDOM wageukia udadapoa’, Gazeti hilo limeripoti kuwa baadhi ya wanafunzi wa kike waliofukuzwa na uongozi wa chuo kikuu cha Dodoma ‘UDOM’ wanadaiwa kugeukia biashara ya uchangudoa mjini Dodoma ili kupata fedha za kujikimu na nauli za kuwarudisha kwao .

Gazeti hilo limeripoti kuwa Juzi kupitia kwa Mkuu wa Chuo cha Dodoma, Prof
Idrisa Kikula kilitangaza kuwasimamisha masomo zaidi ya wanafunzi 7000 wa kozi ya Stashahada ya ualimu ambao hawakuwa na sifa za kusoma masomo hayo.

Gazeti limedai kuwa juzi jioni eneo maarufu la CDA club lilikuwa na idadi kubwa ya kina dada wanojiuza wengi wao wakiwa ni wanafunzi ambao hawakuwa tayari kutaja majina yao.

Post a Comment

Post a Comment