international gossip

POLISI WAANDAMANA NCHINI MAREKANI KWA SABABU YA BEYONCE



Wanachama wa muungano wa polisi na Sherrif walisimama mbali na uwanja wa soka na kuelekeza mwangaza wa bluu katika ukumbi wa tamasha hilo. Walikuwa wanapinga kanda ya video ya Beyonce ambayo wanasema inawaponza polisi.
Mwanamuziki huyo tayari amesema kwamba hawakosoi polisi katika wimbo huo na kusema kuwa maafisa wa polisi wanaodhani aliwaponza wanakosea.

Mwanachama mmoja wa polisi amekiambia chombo cha habari KHOU11 kuwa hawakufurahia baada ya Beyonce kutumia picha za gari moja la polisi mjini New Orleans iliokuwa ikizama katikamafuriko.
“Tunaamini kwamba baadhi ya mambo yake ni kinyume na maafisa wa polisi,” aliongeza.
Mnamo mwezi Aprili, Beyonce aliambia jarida la Elle kwamba anaheshimu polisi lakini hapendi unyanyasaji.

Beyonce alisema “Mtu yoyote anyedhani kwamba siwapendi polisi anakosa kwa sababu.”
“Ninawapenda na kuwaheshimu sana polisi pamoja na familia za maafisa hao ambao hujitolea ili kuhakikisha tuko salama,” aliongeza.
Source: BBC


Jiunge na BONGOHOTZ.COM sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usiache ku download application play store kupata habari ndani ya sekunde kila inapotufikia..Karibu

LIKE PAGE YA BONGOHOTZ KWENYE FACEBOOK



TOA MAONI YAKO HAPA

Post a Comment

Post a Comment