KUTELEKEZA WATOTO/MTOTO.
Ni kosa la jinai. Ni kinyume na kifungu cha 166 cha Kanuni za adhabu. Adhabu yake ni kifungo cha miaka miwili. Kosa linamhusu mzazi, mlezi, au mwingine yeyote aliye na jukumu la kuangalia watoto/mtoto.
KUKATAA KUMPA CHAKULA NA NGUO MTOTO.
Ni kosa la jinai. Ni kutokana na kifungu cha 167 cha kanuni za adhabu. Adhabu yake ni kifungo cha miaka miwili.
KUMNYIMA CHAKULA NA NGUO MTUMISHI.
Ni kosa la jinai. Ni kutokana na kifungu cha 168 cha kanuni za adhabu. Adhabu yake ni kifungo cha miaka miwili. Watumishi wa hapa ni wale wanaotegemea matajiri wao kama wale wa wafanyakai wa ndani n.k.
UKATILI KWA WATOTO.
Ni kosa la jinai. Ni kutokana na kifungu cha 169A cha kanuni za adhabu. Adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka mitano na kisichozidi miaka kumi na tano.
KUHARIBU MTOTO.
Ni kosa la jinai. Ni kutokana na kifungu cha 219( 1 ). Adhabu yake ni kifungo cha maisha.
KUFICHA KUZALIWA KWA MTOTO.
Ni kosa la jinai. Ni kutokana na kifungu cha 218 cha kanuni za adhabu. Adhabu yake ni kifungo cha miaka miwili.
KUJARIBU KUJIUA.
Ni kosa la jinai. Ni kutokana na kifungu cha 217 cha kanuni za adhabu. Adhabu yake ni kifungo cha miaka miwili.
Post a Comment