soka

ARGENTINA YAENDELEA KUSHIKA NAMBA MOJA KWENYE VIWANGO VYA SOKA DUNIANI

Shirikisho la soka duniani, FIFA, Ijumaa hii limetoa orodha yake ya kila mwezi ya timu bora duniani.
Kwenye orodha hiyo timu ya taifa ya Argentina bado inaongoza ikifuatiwa na timu ya taifa ya Ubelgiji na Chile. Ujerumani ni ya 5,ikifuatiwa na Uhispania na Brazil inachukua nafasi ya saba.

Timu ya bara la Afrika inayochukua nafasi nzuri kwenye orodha hiyo ya FIFA ni Algeria iliyopo katika nafasi ya 33 ikifuatiwa na Ivory Coast katika nafasi ya 34.

Kwa nchi za Afrika Mashariki Uganda ipo namba 72;Rwanda 87 Kenya 116 Burundi 122 na Tanzania inachukua nafasi ya 129.

Post a Comment

Post a Comment