Shirika la
Afya Duniani lilikusanya taarifa za sababu za vifo mwaka 2012 na
kuzifananisha na sababu kubwa za vifo mwaka 2000. Magonjwa ya moyo
yamekuwa ni sababu kubwa ya vifo duniani kwani vimesababisha vifo vya
watu milioni 7.4 mwaka 2012. Magonjwa
yasiyo ya kuambukiza kama vile shambulio la moyo, saratani na kisukari
yamesababishwa 68 % ya vifo vyote duniani mwaka 2012, kutoka 60% mwaka
2000.
Ikilinganishwa
na mwaka 2000, vifo vinavyotokana na HIV vimepungua kidogo,
kipindupindu sio tena miongoni mwa sababu tano za juu zinazoongoza kwa
vifo kwani imepungua kutoka vifo milioni 2.2 mwaka 2000 hadi milioni 1.5
mwaka 2012 . Vifo vinavyotokana na kifua vimepungua kutoka milioni 1.3
hadi milioni 1, na kifua kikuu hakipo tena kwenye top ten ya sababu za
vifo.
Top 10 ya sababu zinazoongoza kwa vifo duniani
- Shambulio la moyo 13.2%
- Kiharusi 11.9%
- Pumu 5.6%
- Maambukizi ya njia ya hewa 5.5%
- Saratani ya mapafu na njia ya hewa 2.9%
- Virusi vya Ukimwi 2.7%
- Ugonjwa wa kisukari 2.7%
- Ugonjwa kuhara (Kipindupindu) 2.7%
- Ajali za barabarani 2.2%
- Shinikizo la damu na magonjwa ya moyo 2%
Jiunge na BONGOHOTZ.COM sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook
LIKE PAGE YA BONGOHOTZ KWENYE FACEBOOK
Post a Comment