MAKALA

MAKALA. IJUE TANZANIA NA UTAJIRI WAKE, ILA BADO NI NCHI MASKINI

1.Tanzania ilipata uhuru mwaka 1961 ina miaka 54
tangu ipate uhuru ikiwa ni ya kwanza afrika
mashariki.

2.Tanzania Kwa miaka 38 hii inchi imeongozwa na ccm
peke yake ambayo ni zao TANU na ASP.

3.Tanzania ni nchi ambayo hajawahi kupata majanga
makubwa kama matetemeko ya ardhi,magonjwa
ya mlipuko kama ebola,mafuriko na vimbunga au
ukame.

4.Tanzania ni nchi ambayo imekuwa na kitu ambacho
nnchi za Africa zimekikosa AMANI kwa miaka
yote 54 ya uhuru hajawahii kupigana vita vya
wenyewe kwa wenyewe.

5.Tanzania ina ukubwa ukubwa wa 945,000 km square
yani sawa na uchukuwe Denmark,France,United
kingdom(uk),Netherland,Ireland ujumlishe zote
kwa pamoja.

6.Tanzania ina eneo la bahari lenye ukubwa wa 1,424
kilometers bahari inaleta fursa za usafirishaji,uv
uvi,utalii na nyinginezo.

7.Tanzania ni nnchi ambayo imepakana na nchi za
(Uganda,Rwanda,Burundi,Zambia,Malawi,Drc
congo) ambazo zinategemea bahari yetu kwa
usafirishaji wa mizigo na ni fursa nzuri ya
kuzipelekea bidhaa za viwanda vyetu

8. Tanzania ina maziwa makubwa manne na mengine
madogo mengi.
Maziwa matatu makubwa yako kwenye kumi bora
za ukubwa duniani na Maziwa makubwa matatu
yote yapo Tanzania..Ziwa Victoria ni la tatu kwa
ukubwa duniani(la kwanza afrika) na ziwa
Tanganyika ni la sita kwa ukubwa(la pili afrika)
na la kwanza kwa kuwa na kina kirefu
duniani.Ziwa nyasa ni la tisa kwa ukubwa duniani
(ni la tatu afrika).

9.Tanzania ina mito mikubwa kumi ambayo ni mto
kagera,mto Ruvuma,mto rufiji,mto wami,mto
maragarasi,mto mara,mto pangani,mto mara,mto
gombe,mto mweupe wa nile.na ina mito midogo
mengi kama mto kilombero,mto mbemkuru n.k

10.Tanzania ndiyo nchi ya kwanza afrika kuwa na maji
mengi yasio na chumvi yaliyokuwa kwenye uso
wa dunia(fresh surface water) kutokana na kuwa
na mito na maziwa mengi na kupitiwa na bonde
la ufa.

11.Tanzania ni nchi ya nne kwa uzalishaji dhahabu
afrika baada ya afrika kusini,ghama na mali na
ipo top 20 duniani.
Kuna migodi nane inayochimbwa dhahabu na
miwili imefungwa.
migodi inayochimbwa ni Buzwagi gold mine-
(Shinyanga),Geita gold mine-(Geita),Golden pride
gold mine-Nzega(tabora),Bulyanhulu gold mine-
(Shinyanga).New leuka Gold mine-(Mbeya),
Tulawaka gold mine-(kagera),North mara gold
mine-(mara).Iliyofungwa ni Kirondatal gold mine-
(Shinyanga),Senkenke gold mine-(Shinyanga).

12.Tanzania ina madini ya almasi yanayopatikana
mwadui shinyanga mgodi huo umeanzwa
kuchimbwa tangu mwaku 1940 mbaka leo ado
unachimbwa,unamilikiwa nakampuni ya
wingereza.

13.Tanzania ni nchi ya kwanza na ni nchi pekee
inayozalisha madini ya tanzanite duniani.mkufu
wa kuva shingoni unatengenezwa na tanzanite na
almasi unauzwa hadi milioni 25 za kitanzania.

14.Tanzania ina madini ya chuma yanayopatikana
mchuchuma,ludewa- njombe mgodi unamilikiwa
na wachina mgodi huo una hifadhi ya madini ya
chuma tani milioni 122 ambayo yanawezwa
kuchimbwa kwa zaidi ya miaka 100.

15.Tanzania ina madini ya makaa ya mawe
yanayochimbwa kule kiwira mbeya,mchucuma na
liganga njombe unamilikiwa na wachina pamoja
na ngaka kule mbinga-ruvuma unamilikiwa na
kampuni ya tancoal ya Australia.hifadhi ya
madini ya makaa ya mawe iliyopo ni tani bilioni
2.makaa yam awe ndio chanzo cha pili ya
umeme wabei nafuu duniani baada ya maji.

16.Tanzania ina hifadhi ya madini ya uranium kule
Dodoma(bahi) na mgodi ambao unamilikiwa na
warusi pia madini haya yanapatikana pia
Namtumbo (Mkuju),Galapo, Minjingu, Mbulu,
Simanjiro, Lake Natron, Manyoni, Songea,
Tunduru, Madaba and Nachingwea.

17.Tanzania ni moja ya nchi tatu Africa pamoja
Zimbabwe na madagascar kwa kuwa madini
mengi ya graphite madini haya yapo
Tanga,Mahenge-Morogoro,mererani-
manyara.Madini ya graphite ndiyo yanayotumika
kutengenezea betri za simu,kwenye injini na
brake za gari na kwenye karamu ya risasi
(pencili)

18.Tanzania ina madini ya nickel yanayopatikana kule
kabanga kagera,milima ya ulurugulu-morog
oro,north mara,Ngasoma-mwanza.

19.Tanzania ni nchi ya tatu duniani kwa kuwa na
hifadhi kubwa ya magadi soda mengi duniani
baada ya marekani na uturuki.magadi soda
hutumika kutengeneza vioo vya aina zote vyo
nyumbani hadi magari pia kutengeneza sabuni na
dawa mbalimbali za usafi

20.Tanzania ina hifadhi na mgodi wa madini ya niobium
uliopo Panda hill mbeya ambao ndio utakuwa
mgodi mkubwa wa kwanza Africa na wanne
duniani,mgodi huu unamilikiwa na kampuni ya
uastralia.Madini ya nibioum ni magumu sana
hutumika kutengeneza mabomba pamoja na
madini chuma pia hutumika kutengeneza baadhi
ya sehemu za injini za ndege na vyombo
vinavyoenda nje ya uso wa dunia,vioo vya
computer na lenzi za camera.

21.Tanzania ni nchi ya kwanza Africa na ya pili duniani
kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii duniani ya
kwanza ikiwa brazil. Nchi zilizokuwa kwenye tano
bora kwa utalii Afrika ni Tanzania, Botswana,
Afrika Kusini, Kenya na Zambia.

22.Tanzania ina mbuga zipatazo 16 na ile mbuga
maarufu kuliko zote duniani Serengeti na mbuga
iliyopakana na bahari saadani na mlima mrefu
kuliko wote Africa Kilimanjaro.

23.Nadhani kila Mtanzania anajua juu ya sifa ya
Tanzania kwenye swala ya kuwa na ardhi ya
rutuba inayofaa kwa kilimo

24.Tanzania ina gesi ya asili ya carbon dioxide(CO2)
inayovunwa kule kyejo,rungwe-mbeya na
kampuni ya TOL,gesi ya asili ya cardon dioxide
inatumika sana kutengenezea vinywaji laini kama
soda,bia, na pia kutengenezea madawa,kwenye
viwanda vya makaratasi na kutibia maji.

25.Tanzania ina gesi ya asili inayopatikana katika
kisiwa cha songo songo mkoa wa lindi gesi hii
imekuwa ikichimbwa na kusafirisha Dar as
salaam tangu mwaka 2004 na inayomilikiwa na
kampuni ya songas ya uingereza

26.Tanzania imengundua gasi ya asili yenye ujazo wa
zaidi ya trioni 55.3 cubic meter iliyongungulika
katika maeneo ya bahari ya lindi na mtwara.

Pamoja na sifa zote hizi Lakini Tanzania ni nchi
iliyokwenye kundi la nchi maskini duniani ambao
asilimia kubwa ya raia wanaishi chini ya dola
moja na hali ya huduma za kijamii zikiwa duni.

TA
TIZO NI NINI?NI NANI ALIYESABABISHA HUU
UMASKINI


InstaIour website apps on Google play store @bongohotz 


Post a Comment

Post a Comment