did you know?

Hizi ni rangi ambazo zinapendwa na kunguni!



Watafiti hao, baada ya kufanya uchunguzi wa kina, wamegundua kuwa kunguni hupenda sana rangi zilizokoza zaidi.
Rangi wanazozipenda zaidi ni nyeusi na rangi nyekundu.
Aidha, huchukizwa sana na rangi ya manjano na rangi ya kijani kibichi.
Matokeo ya utafiti huo yamechapishwa katika jarida la kimatibabu la Journal of Medical Entomology.
Matokeo hayo yanaweza kusaidia watu kuwatega na kuwanasa kwa urahisi wadudu hao.
Hata hivyo wanasayansi hao wanasema bado mapema kubaini iwapo shiti za rangi ya manjano zinaweza kutumiwa kuwafukuza wadudu hao kitandani.
Kunguni ni wadudu wadogo sana na hutaka kukaa karibu sana na chakula chao, damu yangu.
Wanaweza kujificha katika godoro, nguo na mianya kitandani. Hupenda pia vitambaa na mbao badala ya plastiki na chuma.
Dkt Corraine McNeill na wenzake walitumia vibanda vidogo vya rangi mbalimbali kwenye maabara na kuchunguza kungini walipenda kujificha wapi.
Walionekana kupenda kujificha katika rangi zilizofanana na miili yao, rangi nyeusi na nyekundu.
Daktari huyo anasema awali walidhani kunguni wangependelea rangi nyekundu kwa sababu damu ni ya rangi nyekundu.
“Hata hivyo, baada ya uchunguzi, sababu kuu tuliyobaini iliwafanya kupenda rangi nyekundu ni kwa sababu kunguni hao wenyewe huonekana wakiwa wa rangi nyekundu, hivyo hudhani rangi hiyo ni kunguni wenzao.”
Huchukia rangi ya manjano na rangi ya kijani kibichi kwa sababu rangi hizi za kung’aa huwakumbusha kuhusu maeneo yenye mwanga ambayo huwa si salama kujificha.
Utafiti uliofanywa awali umebainisha kwamba rangi hizi huwa pia hazipendwi na wadudu wengine wafyonza damu kama vile mbu.
Source: BBC


Jiunge na BONGOHOTZ.COM sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usiache ku download application play store kupata habari ndani ya sekunde kila inapotufikia..Karibu

LIKE PAGE YA BONGOHOTZ KWENYE FACEBOOK



TOA MAONI YAKO HAPA

Post a Comment

Post a Comment