health

HIZI NDIO SABABU ZITAKAZO KUFANYA USILALE SEHEMU ULIYO ZOEA


Je ushawahi kugundua kuwa ukilala katika kitanda au mazingira mapya haupati usingizi wa kutosha?
160426152508_man_woman_sleeping_512x288_bbc_nocredit
Sasa basi, Utafiti umebaini kuwa mtu akilala katika mazingira mapya ubongo wake haulali wote!
Upande wa kushoto wa ubongo huwa uko chonjo dhidi ya hatari yeyote ile, hivyo haulali.
Utafiti huo wa chuo kikuu cha Brown ulioongozwa na Profesa Yuka Sasaki, sasa umeanza kujaribu kutegua kitendawili cha iwapo mtu kama anaweza kuzima upande wake wa kushoto wa ubongo anapolala katika mazingira mapya?
Picha za ubongo wa watu waliojitolea katika utafiti huu zinaonesha kuwa upande huo wa kushoto huwa ukitahadhari endapo patatokea sauti yeyote itakayoashiria hatari.
Utafiti huu ulithibitishwa vilevile kwa ndege na wanyama wengine.
Utafiti mbadala katika chuo kikuu cha Rhode Island umeonesha kuwa ubongo wa binadamu unaweza kubadilika kadri unavyokabiliwa na changamoto mpya.
Aidha Mtafiti huyo Sasaki anasema kuwa dhihirisho la hilo linapatikana kwa watu wanaosafiri kila kukicha.
“Siamini kuwa mtu ambaye analala katika mazingira mapya kila kukicha atakosa usingizi, bila shaka itafikia wakati ambapo atalala tu usingizi wa pono,” alisema Profesa Sasaki.
Source: BBC


Jiunge na BONGOHOTZ.COM sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usiache ku download application play store kupata habari ndani ya sekunde kila inapotufikia..Karibu

LIKE PAGE YA BONGOHOTZ KWENYE FACEBOOK



TOA MAONI YAKO HAPA

Post a Comment

Post a Comment