international gossip
Beyoncé aachia album nyingine kwa surprise, inaitwa ‘Lemonade’, nyimbo zote zina video
0
Comments
Beyonce amepewa jina la malkia wa surprise kwa tabia yake ya kustukiza kwake kwenye mambo mengi anayoyafanya. Mke huyo wa Jay Z ameachia album mpya iitwayo Lemonade, kupitia kipindi maalum kilichorushwa kwenye kituo cha runinga, HBO.
Lemonade inajumuisha nyimbo 12 zenye video zake. Kwenye show hiyo, Beyonce aliongelea kwa mara ya kwanza tetesi kuwa ndoa yake na Jay Z ina matatizo.
Nyimbo za mwisho za album hiyo zinaonesha kuwa aliamua kumaliza tofauti zake na mumewe na kuendelea na ndoa yao. Album hiyo sasa inapatikana kwenye mtandao wa Tidal.
Kwenye moja ya video zake pia wanatokea mama wa vijana wawili weusi waliouawa na polisi, Michael Brown na Trayvon Martin.
Kwenye album hiyo wameshirikishwa The Weeknd na Kendrick Lamar.
Jiunge na BONGOHOTZ.COM sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook
LIKE PAGE YA BONGOHOTZ KWENYE FACEBOOK
Post a Comment