congo

WAFANYAKAZI WA "SAVE THE CHILDREN" WATEKWA NYARA CONGO

Wafanyakazi watatu wa Shirika la msaada la 'Save the Children' wametekwa nyara huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Wafanyakazi hao, wote raia wa Kongo, walitekwa katika jimbo la Kivu Kaskazini majira ya saa tisa mchana jana, hadi sasa hakuna taarifa zozote juu ya walipopelekwa au madai ya watekaji nyara.
Jimbo la Kivu Kaskazini, ambalo lipo mpakani kati ya Kongo, Rwanda na Uganda, lilikuwa kitovu cha mapigano yaliyouwa mamilioni ya watu kati ya mwaka 1996 na 2003. Makundi kadhaa yenye silaha yameendelea kubakia yakiwania udhibiti wa migodi ya madini, na pia kuwaandama raia.

Mwaka jana pekee, watu 175 walitekwa nyara na baadaye kukombolewa kwa malipo, kwa mujibu wa shirika la haki za binaadamu la Human Rights Watch.

Post a Comment

Post a Comment