MAKALA
SIKU YA WANAWAKE DUNIANI AZIMISHENI LAKINI KUMBUKENI NA MAMBO HAYA KATIKA NCHI YETU
0
Comments
Siku ya Wanawake Duniani yaadhimishwa huku Saratani ya Uzazi ikitishia Ustawi wa Mwanamke
WANAWAKE wanaadhimisha Siku ya Wanawake Duniani mwezi huu wa Machi, wakiwa wanakabiliwa na changamoto kubwa inayotokana na vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Saratani ya Uzazi.
Wanawake hasa katika nchi zinazoendelea kama Tanzania, bado wanakabiliwa na matatizo mbalimbali wakati wa kujifungua. Inakadiriwa kwamba kila mwaka kina mama zaidi ya 8,000 hufariki dunia kutokana na matatizo ya uzazi.
Siku ya Mwanawake Duniani ilianzishwa na Umoja wa Mataifa (UN) mwaka 1948. Ugonjwa wa Saratani au Kansa ya Kizazi kwa mwanamke, unaelezwa kwamba ndiyo ugonjwa unaoongoza kwa kusababisha vifo vya wanawake katika nchi zinazoendelea, Tanzania ikiwemo.
Utafiti uliopo unaonyesha kuwa kina mama zaidi ya 500,000 duniani hupatwa na ugonjwa huo kila mwaka. Kati ya hao, wanawake takriban 250,000 hufariki dunia kila mwaka kutokana na ugonjwa huo ambapo hapa nchini takriban wanawake 4,000 hugundulika kuwa na ugonjwa huo kila mwaka. Ugonjwa wa Saratani ya Uzazi umeelezwa kukua kwa kasi, huku waathirika wa tatizo hilo wakiwa ni wanawake vijana wenye umri wa kati ya miaka 25 na 30.
Kwa mujibu wa WHO, asilimia zaidi ya 70 ya visa vya ugonjwa wa Saratani vinaweza kuzuiliwa. Kinachotaki, WHO wanasema ni kwa nchi zenye tatizo hilo duniani kuongeza uwezo wao wa kudhibiti ugonjwa huo wa Saratani.
Hata hivyo, WHO wanabainisha kwamba karibu nusu ya nchi zote duniani, hazina uwezo wa kukabiliana kikamilifu na ugonjwa huo, wala hazina mpango tekelezi wa kuudhibiti ugonjwa huo, mpango unaojumuisha kuzuia, kugundua mapema, kutibu na huduma za uuguzi.
Post a Comment