gossip

NAY ATABIRIWA KUWA MSANII TAJIRI KULIKO WENGINE TANZANIA BAADA YA MIAKA MWAKA MMOJA



Msanii wa muziki wa Hip Hop, Nay wa Mitego baada ya kudai kuwa utajiri wake kwa sasa ni zaidi ya bilioni 1, amedai baada ya mwaka mmoja atakuwa tajiri mkubwa kuliko mtu yoyote Tanzania.
nay new2

Akizungumza katika kipindi cha Weekend Chart cha Clouds TV hivi karibuni, Nay amesema kwa sasa tayari ameshaingia kwa miguu miwili katika biashara ya kilimo.

“Mimi ni mtu ambaye naishi maisha ya ukweli na sijawai kufake, kuanzia mwezi wa sita nimeshaanza kuwekeza, nafikiri hii inaweza ikawa surprise kwa mashabiki wangu. Nimeshaanza kuwekeza katika kilimo, mimi nimeshaanza kununua eka kadhaa pengine panapo majaliwa ikifika mwakani kuna uwezokano wa kuwa tajiri mkubwa kuliko mtu yoyote,” alisema Nay.

Nay alidai kwa sasa nje ya muziki anaingiza pesa kupitia biashara ya daladala.
Post a Comment

Post a Comment