HALI si shwari kwenye familia ya Kampuni ya Endless Fame Productions kufuatia madai mazito yanayomgusa mkurugenzi wake, Wema Isaac Sepetu akihusishwa na kuvunjika kwa ndoa ya mdogo wa mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ almaarufu kwa jina la Esma Platnumz aliyeolewa na Hamad Manungwa ‘Petit Man’.
Mdogo wa mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ almaarufu kwa jina la Esma Platnumz akiwa na mume wake Hamad Manungwa ‘Petit Man’ siku walipofunga ndoa.
MAI NDANI
Katika sakata hilo, mtangazaji maarufu Bongo, Maimartha Jesse ‘Mai’, Esma na Mtangazaji Nasra Rajesh ‘Lady Naa’ wanadaiwa kuunda kundi lenye lengo la kuwasuta wezi wa waume za watu (Wema aliwekwa kwenye tageti) lililopewa jina la Al-Shabaab.
Esma Platnumz akiwa na mume wake Hamad Manungwa ‘Petit Man’.
Wakati mpango huo ukiendelea, Mai anadaiwa alielezea mkasa wa kuvunjika kwa ndoa ya Esma na Petit Man kwenye Instagram huku akimtaja Wema kuhusika kwa mafumbo, jambo lililomfanya staa huyo wa filamu (Wema) aogelee matusi ya kutosha.
MADAI YA WEMA KUHUSIKA
Madai kamili yanamhusisha Wema na uvunjifu wa ndoa hiyo akituhumiwa ‘kuchepuka’ na Petit Man kwa muda mrefu sasa huku mwenyewe akikanusha vikali.
USHAHIDI WA MESEJI
Madai yalizidi kushushwa kwamba, sakata hilo lina ushahidi ikiwa ni pamoja na Esma kubamba meseji zisizo na dalili njema kutoka kwa Wema zikiwa kwenye simu ya Petit Man.
“Ukibahatika kukutana na Esma halafu umkute kwenye ‘mood’ ya kuongea, atakueleza jinsi mume wake alivyokuwa na ukaribu wa kupitiliza kwa Wema. Yawezekana hawakuwahi kuchepuka lakini ukaribu wao ulikuwa wa kupitiliza kiasi cha kuibomoa ndoa hiyo.
SIMU ZA WEMA HADI USIKU WA MANANE
“Esma anadai kuwa kuachana kwake na Petit Man hakuhusiani sana na meseji za Diva (Mtangazaji wa Clouds FM, Loveness Malinzi) kwani hizo zilisherehesha ugomvi wao tu, ila kilichomfanya hadi akaamua kubwaga manyanga ni utitiri wa meseji za wanawake na simu kibao za Wema kumhitaji Petit Man hadi usiku wa manane wakati ni mume wa mtu,” kilidai chanzo hicho.
WEMA ANASEMAJE?
Kufuatia madai hayo, Ijumaa lilimtafuta Wema alipopatikana alisema: “Mimi nimekuwa nikimsapoti Petit kwenye mambo yake na Esma, sasa kama kuna watu wanasema maneno ya kunifanya nionekane mbaya, hao ni watu wasio na nia njema na mimi.
“Nakaa na Petit kama mwanangu lakini pia ni mfanyakazi wa Endless Fame na Esma sina tatizo naye, zaidi watu wanaibua tu mambo yao. Sipendi kabisa…”
ESMA KIMYA
Esma alipotakiwa kufunguka juu ya madai ya Wema kuhusika kwenye kuvunjika kwa ndoa yake alisema kwa kifupi: “Hilo suala liko kwenye ngazi ya kifamilia, siwezi kuliongelea kwa sasa.”
WEMA AKEREKA
Kufuatia maneno ya kuuma kwenye mtandao aliyokuwa akiendelea kuandika Mai, Agosti 18, Wema alishindwa kuvumilia hivyo kwenda kumripoti kwenye Kituo cha Polisi cha Kijitonyama.
Paparazi wetu aliponyetishiwa ‘ubuyu’ huo wa Wema kulifikisha ‘soo’ hilo polisi, alinyanyua mguu hadi kituoni hapo ambapo alikutana na askari wakiongozana na Wema hadi Mitaa ya Sofani, Kijitonyama ambako kuna duka la Mai lakini hawakumkuta hadi kesho yake (Jumatano asubuni) alipotiwa mbaroni.
MSIKIE MAI
Baada ya Mai kufikishwa kituoni hapo alishikiliwa kwa saa kadhaa akihojiwa na alipotoka na kutakiwa kusema chochote kuhusiana na tukio hilo alisema:
“Huu ni mziki mnene, Wema amechokoza moto.”
PETIT MAN NA ESMA
Katika ndoa yao, Petit Man ambaye ni mmoja wa wafanyakazi wa Endless na Esma wamedumu kwa takriban miaka miwili na kujaliwa mtoto mmoja kabla ya mambo kwenda mrama hivi karibuni.
GPL
Post a Comment