psycological advice
MAISHA BAADA YA KUWA MAMA:JE NI MUDA GANI SAHIHI KUKUTANA KIMAPENZI NA MWENZI WAKO BAADA YA KUJIFUNGUA??
0
Comments
Habari yako Kaka wa bongohotz,mm naitwa Pendo,nna umri wa miaka 25 nimeolewa na
nimebahatika kupata mtoto mmoja wa kiume wamepishana mwezi mmoja na siku
moja na Zion huyu ni wa mwezi march tar 15.Napenda kuchukua fursa hii
kukushukuru kwa kutupatia mwanga wa maisha,inshort kwamba wewe ni kioo
changu napenda kuwa kama wewe msikivu, mwerevu, mpenda watu
,muelimishaji rika nk.
Nia na dhumuni la kuandika email hii naomba msaada wako kaka wa bongohotz kuna
watu wanasema kwamba ukisha jifungua hupaswi kukutana na mumeo kimwili
mpaka mtoto atembee la sivyo utambemenda mtoto, wengine wanasema kwamba
unafanya ila ukimaliza pale ukaoge kabla hujamshika wala kumnyonyesha
mtoto la sivyo utamuharibu atakuwa atembei atakuwa kutwa anafanya kazi
ya kuharisha tuu na afya yake itakuwa hafifu kiujumla.Mimi mume wangu
ameondoka mda tangu mimba yangu haija pea yupo UK anasoma na amepata
kazi huko na mwishoni mwaka huu anarudi kuja kuiona familia yake pamoja
na mm mkewe ss hapa ndo najiuliza akija nimwambie tusubiri mpaka mtoto
atembee?na je atanielewa kweli? au kuna njia nyingine safe ya kukutana
na mumeo bila mtoto kuharibika kiafya?nisaidie dada yangu yamenifika
shingoni hata kwa watu niulizie me huwa situmii njia yeyote ya uzazi wa
mpango zaidi ya calendar tu ndio safe kwangu.Pls naomba msaada wa
mawazo.
*Tunaomba msaada wa kimawazo kulingana na unachofahamu.*
ENDELEA HAPA
*Tunaomba msaada wa kimawazo kulingana na unachofahamu.*
ENDELEA HAPA
Post a Comment