sports

WATANZANIA SHUGHULI TUNAYO JUNE 4 NA SEPTEMBER 3


Siku zinazidi kusogea na matumaini ya Tanzania yanazidi kupungua kuhusu safari ya Gabon mwaka 2017 katika michuano ya mataifa ya Afrika. Baada ya timu ya taifa ya Chad kujiondoa katika michuano ya Mataifa ya Afrika na kuacha mtihani Kundi G lenye timu za Tanzania ,
Misri na Nigeria .

March 29 timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles iliondolewa na Misri katika mbio za kuwania kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2017 itakayofanyika
Gabon, Nigeria ilitolewa baada ya kufungwa goli 1-0 katika mchezo wa marudiano.
Jitihada za Ramadan Sobhy kuifungia Misri goli dakika ya 66 ndio zilizoiondoa
Nigeria kwani hawakufanikiwa kusawazisha, Nigeria inaaga mashindano hayo na nafasi pekee inabakia kwa Tanzania na Misri, kwani
Nigeria imebakiza mchezo mmoja dhidi ya Tanzania na hata ikishinda haitaweza kusonga mbele.
Kazi imebakia kwa Tanzania kushinda mechi zake mbili dhidi ya Misri June 4 uwanja wa Taifa na Nigeria September 3 utachezwa Nigeria, kama Tanzania itashinda mechi zote mbili kwa idadi kubwa ya magoli, itakuwa imeizidi Misri kwa tofauti ya magoli. Nigeria ikiifunga Tanzania itakuwa inatimiza point 5 pekee.
Install our website apps on Google play store @bongohotz



Jiunge na BONGOHOTZ.COM sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usiache ku download application play store kupata habari ndani ya sekunde kila inapotufikia..Karibu

DOWNLOAD APPLICATION HAPA..!!


LIKE PAGE YA BONGOHOTZ KWENYE FACEBOOK


Post a Comment

Post a Comment