habari

MREMBO KUTOKA JALALANI 11-----15 - Swahili Viuhapa

featured image





viuhapa

SEHEMU YA 11

Babra alinisimulia mkasa uliompata mpaka nikalia nikamwambia

” Babra wewe si mkosi hata kidogo kwangu wewe ni dhahabu tena ya viwango vya juu”

Endelea

Babra akaniuuliza unamaanisha nini Harrison nikamwambia yeye ni sababu ya mimi kujitambua na kujua nini maana ya maisha

” Wewe pekee ndo unaona hivyo Ila ndugu zangu hawako upande wangu wananiona mkosi”

” Usijali babo tutapambana kwakila hali” 

” Nakuamini Harrison nimekuamini tangu nilipojikuta nipo Salama”

” Usiwaze kilakitu kina sababu”

Siku hiyo ilipita siku ya pili tukajadiliana vitu ndani vimebaki vichache Cha kufanya ni kwenda kutafuta kazi nikamwambia

” Babo hivi wewe unauzoefu wa kazi gani?”

” Yoyote”

” Yoyote inamaana yoyote kazi unafanya?”

” Ndio kwani wewe huwezi?”

” Mimi mwanaume naweza nikafanya kilakazi Sasa wewe…”

” Acha hizo na wewe Mimi nafanya kazi hata Kama fundi ujenzi”

” We acha utani wako bwana fundi ujenzi unausikia tu”

” Haya twende tukatafute alafu uone pigo zangu” 

aliniambia huku akinipigapiga begani Yani Kama katoto vile alikuwa anapenda Sana kucheza michezo ya kitoto nilijua ni uchizi tu kumbe hata tabia yake alikuwa akipenda vimichezo vya kitoto

Tukapanga asubuhi ya siku inayofata twende kwenye saiti moja huko kulikuwa na nyumba inajengwa 

Sikuhiyo ilivyofika tukajiandaa tukasema Leo hakuna kula mpaka tuhakikishe tunapata kazi

Tulitoka kwa miguu tukitembea zetu barabarani bila shida wale wenzangu namimi wakuongea waliongea mpaka mate yakawakauka kooni hatukuwajali tukiwa njiani tukakutana na Asia nikaona nimpe hai tu hata Kama tulipishana ilikuwa ni ubinadamu tu alisema kile kilichokuwa ndani ya moyo wake si dhambi kufikisha hisia zako kwa umpendae nikaona tusiishi kiuadui Mana sio dili

Alitaka kutupita nikaamua tu nimwite

” Asia” niliita hakuitika nilimkimbilia na kumtinga kwa mbele Babo alinifata

” Asia hebu acha kinyongo basi”

” Sina kinyongo na wewe”

” Mbona ulitaka kutupita Kama hutujui vile”

” Naona mgonjwa wako amepona” alipotezea

” Ni kweli lilikuwa ni tatizo la muda tu baada ya kukumbwa na matatizo flani”

” Ooh pole dada” alimwambia Babo

” Asante na nilkushukuru kwa msaada wako wa kuniangalia”

” Kawaida tu usijali” alijibu kitupi

” Asia sisi tumetoka mbali haina haja ya kupigana vikumbo barabarani tusameheane”

” Harrison Mimi sijanuna Ila nilijiskia vibaya kwa kilichotokea Mara ya mwisho nilishindwa hata kukukaribia niliwaza sijui utanifikiriaje”

” Mimi sikufikirii vibaya Wala kuwa na amani tuishi Kama tulivyokuwa tukiishi Kama zamani”

” Sawa Hari mnaenda wapi huku”

” Tunaenda hapo mbele kutafuta kazi”

” Wote?”

” Ndio”

” Sasa kazi gani ambayo mtaifanya wote au kila mtu anatafuta yake”

” Tukipata moja tunafanya wote ikitokea kilamtu akapata yake poa”

” Mnanichosha Sasa Kama kazi ya kuosha vyombo mgahawani mtaosha wote?”

” Ikiwezekana naosha” Basi ukawa utani kidogo

” Unaitwa nani dada?” Alimuuliza

” Naitwa Babo ( Babra)

” Kumbe unajina zuri hivyo Kama unaweza kupika chapati twende ninapo fanyia kazi bosi anatafuta mpishi mzuri wa chapati Mimi napika lakini anahitajika wa pili Mana wateja wapo wengi Sana siwezi kupika chapati nyingi” 

” Chapati naweza Sana tu Kama vipi twende hata kesho”

” Sio kesho sahizi Kama upo tayari”

” Twende”

Ikabidi niwaache waende Mimi nikaendelea na Safari zangu kufika mbele kidogo nikakutana na mzee mmoja akiwa na gari yake

” Shkamoo mzee”

” Marahaba kijana habari yako”

” Salama tu mzee wangu” nikawa, napita

” Kijana!” Aliniita

” Naam mzee”

” Nimepata shida ya tairi hapa nimepata pancha unaweza kunisaidia nikapata fundi anibadilishie tairi” 

Ikawa Kama zari Kama vile Mana kazi hizo nilikuwa naziweza Sana kipindi wazazi wakiwepo nilikuwa nazifanya

” Unajeki mzee wangu” nilimuuliza

” Ndio kwani wewe fundi?” Nikamwambia ndio akasema nitakuamini vipi nikamwambia Kama vifaa anavyo asiwe na shaka

Nikatoa jeki nikatafuta jiwe nikaweka nikaipiga jeki pale nikafungua tairi Mana vifaa alishanipa nikaanza kazi pale Hadi nikamaliza na kufunga tairi nyingine

” Mzee gari yako tayari”

” Unasema kweli?”

” Ndio Kama huamini nipe funguo nikuonyeshe” akasema atajaribu mwenyewe nikamwambia sawa akaingia kwenye gari akawasha akazunguka zunguka nikajua anajaribu ile kufumba na kufumbua mzee anatembelea mbali Sana daah

” Yani kuna watu hawasaidiki Yani nimemtengenezea gari alafu kasepa hata kunipa hata miatano daah” nilijilaumu nikasema Bora ningemtafutia fundi tu ameshanipotezea muda wangu bure

Ndohivyo nikapambana na mwendo mpaka nilipofika kwenye hiyo nyumba iliyokuwa ikijengwa nikamkuta msimamizi pale

” Kwema ndugu?” Nilimsalimia akageuka daah kumbe Peter ndiye alikuwa msimamizi pale aliponiona tu akabadilika sura

” Nimekusalimia Peter”

” Poa”

” Sikutegemea Kama wewe ndo msimamizi hapa”

” Mimi ndo nipo hapa”

” Sawa Mimi nahitaji kazi ya usaidia fundi”

” Hakuna kazi hapa kila fundi anamsaidizi wake”

” Jamaa yangu hakuna hata kazi ya kujaza kifusi”

” Aisee Harrison mbona Mimi najuaga wewe ni mwelewa Sana imekuwaje hujaelewa niliposema kazi hakuna?”

” We ni jamaa yangu bwana huwezi kosa mahali pa kuniweka!”

” Harrison Kuna ujamaa Kuna kazi nadhani unaelewa Mimi Sina ujamaa kwenye kazi za watu”

Peter alinikatia Mara alikuja jamaa mmoja fundi akamuita Peter

” Peter bosi wako kaja anakuita”

” Oya Hari we nenda katafute kazi kwingine acha nikaonane na bosi”

Nikamwacha Kama alivyo nikawa naondoka kuja kucheki mbele nikaona ile gari iliyonikimbia nikasema hapa nakula nae sahani moja lazima anipe changu nikasogea mpaka pale nikawa naangalia Kama kuna mtu ndani lakini hakukuwa na mtu 

Nikasema acha nisubiri palepale mpaka aje nilikaa Kama lisaa na nusu ndo akawa anatoka akiwa na Peter nikaona peter anamuaga kazi njema bosi

” Kumbe huyu ndo bosi hapa Sasa kwanini hajanilipa na kanikimbia” nilijiongelesha mwenyewe nilisubiri Peter alipoondoka ndipo nikamfata mzee

” Mzee”! Nilimwita

” Hee ni wewe kijana haki ya mzungu Yani kukukwepa kote tumekutana hapa!” Alicheka sana

Nilivaa sura ya kazi sikuonyesha jino Wala kuchezesha pua Yani mimi nimekasirika alafu yeye anacheka utafikiri ametekenywa unyayo

Ghafla mzee akaanza kushika kifuani akawa anahema kwashida akiyumba

” Nini mzee wangu unashida gani?”

Hakuweza kunijibua alitoa macho tu akionyesha kidole kwenye gari lake nikamshika na kufungua mlango wa gari nikijua alitaka akae kwenye gari baada ya kumuingiza tu akapeleka mkono mbele na kutoa kakitu fulani na kukaweka puani baada ya muda kidogo hali yake ikabadilika nilimwacha atulie kwa muda 

” Asante kijana bila wewe hali yangu ingekuwa tete Sana nisingeweza kufika ndani ya gari”

” Kwani tatizo nini?”

” Athma ilinibana Sana na hii ndo dawa yangu siku zote natembea nayo”

” Pole Sana na kwanini usitafute dereva awe anakuendesha hata unapopatwa na shida Kama hii uwe na mtu karibu?”

” Hata daktari alinishauri hivyo Sasa sijapata mtu mwaminifu”

” Maaminifu wapo Ila umeshindwa kuwapata kwasababu wewe mwenyewe hujiamini ni ngumu kumwamini mtu”

” Hapana kijana Mimi najiamini”

” Ungekuwa unajiamini unganilipa baada ya kufanya kazi yako badala yake ukanikimbia huenda hujaanza kufanya kwangu nandio maana watu wanakukwepa sio Kama hujampata sema wanakukwepa”

” Huenda ni kweli?’

” Huo ndo ukweli ungekua hujanikimbia ningekuwa dereva wako mzuri mpaka ungependa Ila kwakuwa huaminiki acha yakukute” nilitaka kuondoka

” Ngoja,ngoja,ngoja usiondoke”

” Unanilipa au?”

” Nakupa” alitoa elfu20 akanipa

” Hapa sawa Mimi naenda”

” Mbona hatujaelewana Sasa!”

” Kuhusu nini?”

” Umeniambia kitu kizuri alafu unataka kuondoka? Usiondoke tuongee” nilirudi

” Tuongee nini mzee?”

” Kwanza Leo nataka unipeleke nyumbani nitakulipa alafu nataka uwe dereva wangu kuanzia kesho unaleseni lakini?” 

Nikamwambia ninayo akaniambia Basi kesho uje uanze kazi na hivi karibuni Nina Safari ya mkoani huko mbeya tutakuwa wote

Nikaingia kwenye gari nikawasha nikampeleka mpaka kwake akanikaribisha ndani kabisa nyumba yake ilikuwa vizuri kiufupi alijiweza

Nikamkuta mkewe na watoto wao wa kike tukasalimiana pale akaniambia

” Kijana naomba utizame macho yako chini na yasiwe kwa binti zangu Mana nyie vijana wa sikuhizi hamna adabu” nikamwambia ondoa shaka macho yangu nitayaweka mfukoni wote wakacheka Sana

Akawaambia mkewe pamoja na mtoto wao kuwa Mimi ndiye dereva wake na ikitokea dharura ya Safari yoyote basi nitawajibika na Safari hiyo haijalishi ye ye au mkewe au mtoto pia

SEHEMU YA 12

Akawaambia mkewe pamoja na mtoto wake na ikitokea dharura ya Safari yeyote basi nitawajibika na Safari hiyo haijalishi yeye au mkewe na mtoto pia

SONGA NAYO

Baada ya hapo nikarudi zangu nyumbani nikapika ugali tu Mana ilichafika mchana nikala pale uliobaki nikamwekea Babra mida ya tisa mchana Babo alirudi kutoka huko kazini walikoenda na Asia

” Hari umeshindaje?”

” Poa vipi wewe”

” Niko powa”

” Vipi kazi”

” Kazi Safi nashukuru kufika tu nikapewa kazi ya chapati nahivi sijapika kitambo nahisi mgongo na kiuno vyote havina kazi”

” Pole”

” Asante Ila njoo tu unikanyage mgongo labda utapoa”

” Yani na uzito huu nilionao unataka nikukanyage mgongo si nitakuvunja?”

” Baba weee ulivunja wangapi Yani hufai kuwa hata dokta”

” Ndomana sikuwa Mana kubembeleza sijuagi” ulikuwa ni utani tu nikaenda nikamkanyaga kanyaga pale maisha yetu tulisha yazoea chakula kikibaki Kama mboga unapasha Basi unapiga diko akala na yeye Sasa tukakaa Sasa

” Haya niambie huko ulikoenda imekuwaje?”

” Aah Safi japo nilikutana na mzee mmoja mwenye Mambo ya vijana Ila tumeenda sawa nimapata kazi ya udereva”

” Safi sana”

” Wewe vipi?”

” Kuhusu?”

” Kazi”

” Anhaa daah kazi bwana ikopoa Ila mshahara ni elfu tatu kwa siku”

” Mbona ndogo”

” Harrison sio ndogo kwetu ni ndogo kimahesabu ya haraka lakini ukipangilia inatosha”

” Sasa hapo unapangiliaje”

” Sikia Mimi mchana nakula kazini wewe unakula huko kazini kwako usiku vitu vipo elfu tatu tunaweka kwenye kibubu tukipata shida basi tunatoa mpaka wewe utakapo pata mshahara wa mwisho wa mwezi hizi elfu tatu tatu hazitatusaidia?”

” Wanawake mnamahesabu Sana yani enzi zangu hiyo elfutatu Kama ya maji tu”

” Khaa Yani wewe ndomana ulishuka Mana ulikuwa uanatumia pesa bila mahesabu alafu ulikuwa na kazi kweli wewe”

” Nitoe wapi nilikuwa nakula za urithi”

” Baada ya kwisha”

” Kama unavyoniona hata wale inzi waliokuwa wakitua kwenye mabaki ya vyakula nao walihama” Babo alicheka sana

Siku sikawa zinasonga babo akiendelea na kazi Mimi nikiendelea na kazi yangu ya udereva na tukiwa tunaishi ndani ya chumba kimoja Yani tunapishana muda wakuoga na kulala yeye analala kitandani Mimi nalala chini

Mwezi ulipita tangu tupate kazi bosi wangu alinipa mshahara laki mbili nilipofika nyumbani siku hiyo nikamkuta Babra ameshatoka kazini 

” Vipi Babo?”

“Poa tu” aliitika kinyonge

” Vipi unaumwa?”

” Hapana nipo sawa”

“Mbona kinyonge Sana”

“Harrison nawaza kwakipindi chote tuko pamoja sijapata taarifa zozote kutoka nyumbani sijui watakuwa wazima wote aula”

” Hilo ndo linakupa shida?”

” Ndio unajua yaliyotokea mimi nimesamehe wale ni wazazi wangu napata hofu Sana nisipo jua taarifa zao”

” Sikia Mimi wiki ijayo naenda mbeya bosi wangu anasafari ya kule ya kibiashara Kama vipi nielekeze kwenu mimi nikawajulie hali alafu niwape taarifa zako”

” Mmh”

” Vipi unahisi bado watakuwa wanahasira na wewe?”

” Sina hakika Ila labda uende tu usiwaambie habari zangu wewe waangalie Kama wapo salama”

” Poa usijali”

Babo akaniambia kwamwezi mzima amepata elfu tisini Mimi nikamwambia nimepata laki mbili akasema kwanini tusinunue mbao hata chache kwanza kwaajili ya kuanza kupaua nyumba Mana tumeishi kwenye chumba kimoja muda mrefu kwasababu hatukuwa na kazi nikaona mbona wazo zuri kweli nikaenda kutafuta mbao nikapata ambazo walinipiga hesabu ya nyumba yote wakaniambia kwasababu ni Mimi watanifanyia laki nane na nusu nikaomba niwe nalipia kidogo kidogo alafu nikimalizia wanipe Basi nikatoa ile laki mbili na tisini nikawaomba niwe napeleka kidogo kidogo mpaka nitakapo maliza wakakubali

Ilipita wiki Sasa Safari ya kwenda mbeya iliwadia 

” Harrison nakuombea usafiri Salama “

” Sawa Ila na wewe ubaki Salama jitahidi kufanya kazi Sana akasema sawa tukaagana pale nikaondoka na gari siku hiyo nilimuomba bosi wangu twende na gari yangu Mana ilikuwa ipo tu akakubali 

Safari ilienda Salama tu tulifikia hotelini bosi alichukua vyumba viwili changu na chake akaniambia Harrison wewe kalale Mimi nitakuwa na kikao usiku huu nikamwambia sawa Ila muda wa kulala ulikuwa bado nazunguka zunguka kwanza akasema sawa 

Nikachukua gari nikatoka pale hotelini nikatembea mwendo kidogo nikaona briefcase yake ameiacha ikabidi nigeze gari mpaka hotelini

Nikaulizia wahudumu pale wakaniambia huyo mzee ameingia kwenye kikao nikamwambia nahitaji nimpe briefcase yake akasema Mimi siruhusiwi kuingia ndani labda nikupeleke kwa mtoto wa mtu ambae ndo yupo nae kwenye kikao na ndo mwenye hoteli nikasema utakuwa umenisaidia

Tukatoka pale mpaka ofisini kwa huyo mtoto wa bosi wake aligonga mlango ulifunguliwa akaingia na kutoa maelezo ndipo na Mimi nikaruhusiwa kuingia 

Niliingia na kukutana na kijana Marika yetu hayakupishana saaana japo kwamuonekano Mimi nilimzidi kidogo

” Karibu” alinikaribisha

” Asante habari za kazi?”

* Safi tu “

” Nimeambiwa shida yako weka hapo wewe nenda” nikaweka mezani ile briefcase nikatoka nikaona nisiendelee na kwenda kuzunguka mtaani niende zangu kulala wakati nataka niingie kwenye chumba changu nikaitwa

“Kaka!” Nikageuka alikuwa ni mwanamke 

” Samahani naomba msaada wako” aliniambia

” Msaada?”

“Ndio Kuna vitu nimeshindwa kushusha kwenye gari nimempigia mtu simu naona Yuko bize”

” Sawa”

Tukaongozana mpaka kwenye gari yake nikamsaidia kushusha pale 

” Asante Kaka “

” Haya”

” Unaitwa nani Kaka”

” Naitwa Harrison”

” Ooh sawa upo hapa kibiashara au”

” Hapana Mimi ni dereva nipo na bosi wangu yeye ndo yupo hapa kibiashara”

” Mmh Yani kwa muonekano wako mtu hawezi kudhani wewe ni dereva wa mtu uko vizuri Sana” nikachulia poa tu nikamwacha amesimama Mimi nikaingia zangu kulala

Nikiwa kitandani nilikumbuka ombi la Babo la kwenda kwao Mana alishanielekeza nikatoka nikaenda kwa muhudumu mmoja na kumuulizia huo mtaa akaniambia mbona sio mbali hata kutoka pale hata nikitembea kwa miguu nafika

Nikaondoka kuelekea huo mtaa kwajinsi nikivyoelekezwa nilifika nikaulizia ulizia pale kwa mzee mwaipopo ni wapi wakanionyesha

Nikaenda na kugonga geti alitoka mlinzi

” Nani wewe”

” Naitwa Hari!”

” Nikusaidie nini”

” Mwenye nyumba nimemkuta”

” Nani manamke au mwanaume?”

” Yoyote”

” Mwanaume hayupo ila yupo mama”

“Hata huyo nikimuona si mbaya”

” Subiri hapa nikampe taarifa”

Nikasubiri pale baada ya muda alikuja

” Ingia” aliniambia nikaingia akanisindikiza mpaka mlangoni nikagonga na kuitikiwa nikaingia mpka ndani nikamkuta mama wa Kati ya miaka hamsini au hamsni na

Nilimsalimia akaitika akaniuliza Nina shida gani nikamwambia Mimi nilisomaga na Babo kwanza akashtuka akaniambia nimetokea wapi nikamwambia niliendaga dar ndo nimerudi akasema

” Nasikitika Sana”

” Kivipi mama?”

” Huyo Babo hapa hayupo”

” Yuko wapi”

” Sijui atajua mwenyewe huko aliko sijui anauza baa wapi Mana hakuna anauejua Wala kuhitaji habari zake afadhali hata alivyoondoka”

Maneno ya mama yalinisikitisha Sana kwauelewa wangu nilijua mama ni mtu wa huruma Sana kuliko baba Mana ndiye anajua uchungu wa mwana lakini yeye bila haya wala huzuni yoyote alijibu kirahisi tu nilimuona mama wa ajabu Sana kiufupi niliwaona ni wazazi ambao hawastahili kabisa

Nikajisemea tu haina haja ya kumwambia habari za Babo nikaaga na kuondoka zangu kurudi hotelini

Moyoni nikasema Mimi ndio kilakitu akitoka mungu Mimi ndiye nafata kwenye maisha yake 

Kama wazazi wake wamemkatia tamaa Mimi nitapambana na kuhakikisha anapata kilakitu na atakuwa na furaha na asijiskie upweke

Tulikaa pale hotelini kwa siku Kama nne hivi bosi wangu akaniambia biashara yake imeisha kwahiyo nijiandae turudi dar nikasema Mimi nipo tayari

Usiku huo sikulala mapema nikawa nimekaa tu nje ya hoteli nikishangaa mazingira ya pale na kuangalia watu wanavyoingia na kutoka nikiwaza na Mambo niliyoyasikia kwa mama Babo na nilifikiria jinsi nilivyokutananae kwa hali aliyokuwa nayo nikasema Kuna Sababu ya Babo kuja kwangu mbona alipita nyumba nyingi tu lakini alifikia kwangu na hata nilipomtimua alirudi

Nikasema Babo wewe ndo mwanamke wa maisha yangu tutapambana kwakila hali tutafika mbali dunia itashangaa niliiambia nafsi yangu

Ukitaka kulipia nijulishe WhatsApp au inbox kwa namba ya malipo voda ni 0754201697 TIGO 0710809556 jina adelina ndimbo na Namba ya WhatsApp ni 0710809556

Tukutane sehemu ya 13 

MREMBO KUTOKA JALALANI

SEHEMU YA 13

Nikasema Babo wewe ndo mwanamke wa maisha yangu tutapambana hali tutafika mbali dunia itashangaa niliiambia nafsi yangu

ENDELEA

Nikiwa nawaza yangu Mara yule Dada noliyemsaidia kushusha mizigo alikuja

” Harrison au nimekosea?”

” Hujakosea za tangu siku ile”

” Salama nilijua umeshaondoka”

” Naondoka kesho”

” Hee jamani si mngekaa hata mtembee tembee uijue mbeya vizuri”

” Bosi ameshamaliza shughuli zake inabidi tuondoke”

” Nipe hata namba zako basi”

” Sina simu”

” Acha utani wako yani kwa uhandsomel wote huo simu huna?”

” Ndio Sina “

” Unaniaibisha sasa wifi unawasiliana nae vipi?”

” Aah…bado sijampata” sikutaka nimweleze kilakitu

” Kumbe daah ingekuwa poa Sana Kama ungekuwa na simu we kwako wapi” 

” Kwetu ni dar”

” Sawa mume wangu anakujaga huko Mara kwa mara”

“Mume wako?”

” Ndio ambae ndo mmiliki wa hii hoteli”

” Kumbe au ndo yule nilimuona kwenye ofisi flani”

” Yukoje Mana hapa kuna ofisi nyingi Ila ofisi kuu ni yake”

” Mrefu kidogo mtanashati hivi”

” Ooh ndo yeye ila wewe ni handsome zaidi”

” Kawaida sio sana” akacheka

Nikainuka akaniuliza mbona unaondoka nikamwambia naenda kulala ili niwahi kuamka mapema

” Kwahiyo kweli huna simu?”

” Sina sikutanii”

” Daah haya bwana vipi umeshakula?”

” Ndio tayari”

” Twende basi ukapate hata soda baridi”

” Asante siku nyingine Leo Niko fulu”

” Jamani hata soda?”

” Usiwaze nitakunywa siku nyingine”

” Tutaonana wapi?”

” Milima haikutani Ila binadamu hukutana”

” Bado unaamini hiyo misemo?”

” Naamini kwasababu ndivyo ilivyo kwani ulitegemea utakutana na Mimi?”

” Hapana”

” Inawezekana tukakutana sehemu nyingine tofauti na hapa Mana sisi bado ni vijana na bado tunatafuta maisha “

“Lakini kweli haya acha nikutakie Safari njema”

Nikatoka pale ili niende kulala Mara nikamuona bosi akiwa mlangoni kwenye chumba changu

” Kumbe ulitoka?”

” Ndio”

” Hata Mimi nilitoka”

” Mbona hukusema nikupeleke?”

” Ujue Mimi ni mzee Kuna Mambo nyinyi vijana hamtakiwi kujua ndomana nikaenda mwenyewe”

” Haya mzee ulikuwa unasemaje?”

” Nimekuletea simu hii naona Kuna siku nitakuhitaji ghafla nikashindwa namna ya kukupata kitambulisho si unacho?”

” Ninacho?”

” Basi hakikisha unasajili laini pindi tukifika Dar Mana mwezi huu nitakuwa na pilika pilika Sana”

” Sawa mzee”

Ilikuwa ni simu ndogo aina ya itel yeye akarudi chumbani kwake mi nikaenda chumbani kwangu

Asubuhi tukaanza Safari ya kwenda dar tukifika majira ya usiku nikampeleka bosi kwake akanpa hela Kama posho nikaenda zangu nyumbani

Nilifika Babra alikuwa tayari ameshafunga nikagonga mlango nikaskia anafoka

” Nimesema toka kabla sijakuitia watu huna hata haya kwani nilikuambia ninashida na pesa zako mbona hamkuja kipindi ambacho nilikuwa nazurura barabarani? Nimesema tokaaa!!” Alisema Babra Tena Kama Alikuwa analia

” Babo ni Mimi Harrison”

“Hee!? Alishtuka nikasikia anatembea kuufikia geti alifungua Kisha nikaingiza gari

” Karibu Harrison”

” Asante “alinipokea begi dogo nililokuwa nimebeba tukaingia ndani

” Pole na Safari”

” Asante vipi hali yako?”

” Salama” aliitika akigeukia pembeni alijifuta uso

” Mbona unalia babo?”

” Wala silii nilikuwa najiminya chunusi ikawa imeuma mpaka nikatoa chozi”

” Mmh ndo ulie?”

” Sijalia kweli’

” Na ulikuwa unamfokea nani”

” Ah… nili.. nili.. nilikuwa naongea na mtu alikuwa anapita huko nje”

” Kweli?”

” Ndio vipi umekula?”

” Nilikula mchana njiani”

” Ngoja basi nikupashie tambi ule”

” Kwani za baridi Sana?”

“Ndio”

” Au acha tu Babo nitakunywa asubuhi na chai”

” Utalala njaa”

” Wala hata haiumi Sana”

“Kuoga je?”

” Kuoga sawa” Babo akachukua ndoo ya bafuni 

” Hiyo ndoo unapeleka wapi”

” Kukuwekea maji”

” Acha bahna Babo naenda nayo mwenyewe”

” Umechoka Hari acha nikaweke”

” Babo “

” Bee!”

” Njoo ukae hapa” nilimuonyesha pembeni yangu

” Hapo?”

” Ndio”

Alionekana kuwa na hofu

” Unaniogopa?”

” Wala!”

” Mbona Kama hujiamini?”

“Mi nakuonea aibu bahna kaa kule mwisho Mimi nikae hapa”

” Leo hii?”

” Ndio ” nikasogea

” Nilifika mpaka kwenu”

” Kweli?”

” Ndio”

” Uliwaona mama na baba?”

” Nilimkuta mama tu naona baba alikuwa kazini”

” Eeeh jamani mzima lakini”

” Mzima wa afya”

Babo alionyesha kufurahi Sana niliwaza kwa furaha aliyokuwa nayo nitaanza vipi kumwambia maneno ya mama yake aliyoyasema juu yake si atakuwa mnyonge Sana na Mimi siwezi kuvumilia kuona anaumia aliuopitia yanatosha Mana kichaa huwa anapitia mengi magumu nihivyo akili zake zinakuwa kwenye Giza na kuona kilakitu sawa haya Sasa amepona Tena akutane na maumivu hapana acha iwe Siri yangu acha nisimwambie isije akaweka chuki na wazazi wake Mambo yanaishaga acha nimwaminishe wazazi wake wanampenda ipo siku mambo yatakuwa sawa

” Harrison ulinimuambia wewe nani”

” Classmate wako”

” Alafu”

” Nikasema Babo nimemkuta”

” Akajibuje”

” Akasema hayupo hata hatujui aliko Yani sijui atakuwa katika hali gani”

Babo alifurahi mnoo si mchezo akaniuliza Kama nimemwambia kuhusu yeye nikamwambia hapana kwasababu ningekuambia huenda angenishtaki kwa kukaa na mwanae kwa kipindi chote bila kutoa taarifa babo aliamini tu

” Yani nitafanya kazi kwa bidii nataka mwezi wa kumi na moja twende wote mbeya”

” Wote?”

” Ndio mama arafurahi na atakushukuru sana kukaa na Mimi vizuri” maskini nilimuonea huruma bure Mana alichokifirahia hakikuwa kweli ukweli niliuficha Ila niliona ni njia sahihi ya yeye kutokuwa na mawazo kuhusu wazazi wake na kuondoa chuki kwao 

” Babo”

” Bee”

” Unawapenda Sana wazazi wako?”

” Sanaa yani nawapenda huwezi amini Yani Yale yote yaliyotokea moyoni yameondoka na nimehisi mzigo nimeutua Yani nitapambana sitaki niende nyumbani mikono mitupu nataka wakaone kweli mtoto wao nimekua mpambanaji”

” Niahidi kitu Babo”

” Nini Sasa”

” Chochote”

” Mmh nakuahidi… Hapana ahadi sio nzuri”

” Kwanini?”

” Sisi wanadamu tuna ahidi Kama vile tunajua tutaishi muda gani”

” Kwahiyo ahadi ni mbaya?”

” Ahadi sio nzuri Wala sio mbaya Ila Mimi nahitaji kuweka Nia ndani ya moyo wangu “

” Nia ya nini?”

” Nia ni Siri Hari ila ikitokea nitakuambia”

” Unamasihara wewe Mimi nataka nikuahidi”

“Sitaki uniahidi”

” Kwanini?

” Naogopa ahadi Mana nyingi huwa hazitimii Bora uweke Nia ndani ya moyo wako kwasababu Nia hufanya ahadi kutimia unaweza kuweka ahadi kumbe huna Nia ya kutimiza ahadi”

” Kwahiyo unataka kuniambia kutimiza ahadi mpaka uwe na Nia”

” Ndio hivi unajua Kuna watu wanaahidi tu lakini sio kwamba wanamaanisha na wengine hutimiza ahadi kwasababu fulani na wanaahidi ili kupata kitu fulani?”

” Haya nimekuelewa cheupe”

” Haya kaoge”

” Naona leo nimakuwa mtoto umenikumbusha mbali Sana kipindi mama yupo nikiwa mdogo nilikuwa nachezaa ukifika muda wa kuoga nakimbilia kulala basi utaskia mama anasema harri haya kaogee”

” Kwahiyo nimekuambia Kama mtoto?”

” Hapana Ila umenikumbusha mbali Sana”

” Haya Ila kaoge kwanza ” nikachukua kindoo nikaenda zangu kuoga nakuvaa zilezile nikarudi ndani nikatandika chini nikalala

Asubuhi yake Babra alienda kazini Mimi siku hiyo sikuwa na ratiba ya kutoka nikafanya usafi nikapika chai nikanywa nikaingiza mkono mfukoni na kutoa zile hela alizonipa bosi nikahesabu zilikuwa ni laki na nusu nikasema ngoja nikapumguze ela ya mbao na bati Sasa ile natoka Babo nae akawa anakuja 

” Kulikoni mbona mapema?”

“We acha tu eti bosi kanisimamisha kazi kwasababu eti Kunapesa zimepotea baada ya Mimi kuingia nilipoenda kuchukua unga”

” Kwani mlikuwa wangapi?”

” Mimi na Asia na wahudumu wengine”

” Kwahiyo wakati unaingia bosi alikuwa wapi?”

” Alikuwa ndani lakini baada ya Mimi kutoka aliingia Asia ndipo akaja kuniambia kuhusu pesa kuibiwa na bosi akaniita akasema Mimi ndo nitakuwa nimechukua pesa”

” Nikamwambia sijachukua Yani Hadi nilivua nguo zangu anisachi lakini hakuamini akasema wote niliowakuta pale Wana miaka haijawahi kutokea yeye kupotelewa na pesa kwanini Mimi niingie tu na pesa kupotea”

” Pole Babo kwahiyo?

” Ujue nini hari inavyoonekana Kuna watu hawataki nifanye kazi pale Mana Kuna vitu vingine hata sielewi “

” Kivipi?”

” Kuna siku niliweka unga ili nianze kukanda Sasa nikawa nimesahau chumvi nikaenda kuchukua chumvi na kuanza kukanda unga nikapika chapati vizuri wateja kula eti chumvi ikawa nyingi hata nilipoonja Kama vile nimeweka pakti nzima Hadi nikashangaa”

” Hapo naamini Sasa itakuwa ni Nani?”

” Hari Mimi siwezi kumhisi mtu ikiwa hakuna Hata niliyegombana nae labda nimgesema ni yeye”

” Daah Ila binadamu tuna mioyo ya ajabu Sana”

” Ulikuwa unatoka unaelekea wapi?”

” Naenda pale hardware nataka nikapumguze deni”

” Hebu subiri twende kwanza ndani”

Tulirudi mpaka ndani

” Harrison hivi huwezi pata mahali ukaazima pesa”

” Pesa za nini?”

” Mimi nimewaza kitu unapajua pale Kona kwa yule mama aliyekuwa na panda la mkaa?”

” Namjua “

” Pale Kuna Banda lingine ambalo lilikuwa ni genge nikawaza kwanini tusifungue genge pale Mana ule mtaa wote pale hakuna genge wanategemea kule kwa mzee bakari”

” Genge si linahitaji mtaji mkubwa”

” Hata ukiwa na laki moja unaweza kuanzia Mana genge linajizalisha lenyewe”

” Kwahiyo laki inatosha”

” Inatosha kwa kuanzia”

” Poa Mimi nakupa hiyo laki Mana nilikuwa na laki na nusu nilitaka kwenda kulipia mbao na bati”

” Fanya Kama umenikopesha Mimi nitakurudishia pindi nikapata mtaji utakao simama wenyewe”

” Poa” nikampa laki moja ile nikabakiwa na elfu hamsini na yeye alikuwa na akibakama elfu kumi na tano hivi akaongezea nikaahirisha kwenda kulipia mbao tukaenda kuangalia Banda chakushukuru tukampata mwenyewe akakubali kutukodishia kwa elfu thelathini tukampa hela ya miezi miwili akasema anatoa wiki mbili tumpe hela yake yote iliyobaki tukaondoka kwasababu ilikuwa bado mapema

Nikachukua gari nikatoa siti tukaenda sokoni tukanunua mazagazaga ya laki ikaisha tukarudi kesho yake tukaenda kuweka kibanda sawa tukapanga vitu nikamwacha pale nikarudi nyumbani

Nikaingiza gari Sasa ile nataka niingie ndani naskia mshindo upande wa nyuma ya nyumba ile iliyoungua kwenda kucheki imebomoka Kati kwa kati

SEHEMU YA 14

Nikaingiza gari Sasa ile nataka niingie ndani naskia mshindo upande wa nyuma ya nyumba ile iliyoungua kwenda kucheki imebomoka Kati kwa Kati

ENDELEA

Nyumba ilipomoka yani ilijitenga nusu kwa nusu ukawa msiba mwingine Yani najiandaa kupaua nyumba inaanguka duuh kwanza nikakaa chini kuangalia vizuri Kama ninachokiona nikweli Mana akili ilivurugwa daah

Ikafanya nikumbuke maneno ya baba sikumoja tulitoka kifamilia tukaenda hoteli moja hivi ipo kibaha maili moja inaitwa kiba conference nikaona gari moja Kali nikamwambia baba aninunulie gari Kama ile akaniambia

” Harrison mwanangu naweza kununua vingi vya thamani nikakupa lakini nitakuwa sijakusaidia” nilipomuuliza baba kwanini akaniambia

“Ukiwa na kitu kichwani ni muhimu kuliko ulichoshika mkononi Mana muda na saa yoyote chaweza kukuponyoka” sikumuelewa nikamuuliza maana yake akasema

“Maana ya Mimi kukupeleka gereji nataka uwe na ujuzi ambao utadumu kwako daima utatumia kupata kile unachostahili mwanangu lakini nikikuachia Mali Kama huna akili ya kuzitunza itakuwa ngumu Ila jitahidi Sana kutumia akili kupata chako ila pia tunza ulichonacho nikusaidie badae unajua nini Harrison Mimi na mama yako tulikuwa tunapamba kwelikweli na hata tulipopata kikubwa hatukukisahau kidogo chetu hatukuwa na tamaa na vya watu kwasababu hatukujua wamepataje na siku zote usimchukie mtu kwa hali au mafanikio yake maana hujui amepitia mangapi na usione asiyenacho ukasema ni mzembe ila kupata pia nimajaliwa”

Sasa nilielewa maneno ya baba wanasema neno ningejua huja mwisho wa Safari ndo Mimi huyo nilikumbuka jinsi nilivyokuwa nikila bata za kutosha kilicholala kwangu kilikuwa haramu masikini niliona sio watu kumbe nilikuwa nakosea

Niliegemea ukuta wa fensi nikajikuta nalia Yani Kama ilikuwa ni adhabu kwangu nikasema kweli mtegemea Cha nduguye hufa masikini ingekuwa nimetunza Mali na kuziendeleza leo ningekuwa mtu wa tofauti ona nataabika kwa ujinga wangu

Basi nikakaa pale nikaona ishu ishakuwa nzito kinachotakiwa nikuanza upya ujenzi pesa Sina nikasema labda nikachukue tu pesa nilizo Anza kulipia mbao na bati 

Nikaenda mpaka kwa yule jamaa niliyempa pesa nikamkosa nikamuulizia niliyobiwa yalikuwa makubwa

” Yani huyo jamaa hivi ninavyokuambia anatafutwa kakimbia na hela za watu kibao”

” Kwani yeye sio mmiliki?”

” Siyo yule alikuwa ni msimamizi tu hapa Yani mwenyewe Jana nimelipia bati za milioni tatu nikamwambia leo nakuja na gari kuchukua Mana aliniambia magari yake yapo kwenye tripu za mikoani Sasa leo nimekuja kuchukua naambiwa katoroka”

” Ametoroka saa ngapi”

” Kwenye saa tano asubuhi”

Nikaona ishakuwa balaa kumbe Mimi nalia na Malaki wenzangu wanalia na mamilioni eeh nikaamua nirudi zangu ndo hivyo nishaingia Cha kike basi nitafanyaje

Nikafika nyumbani nikaingia ndani kujitupa kwenye kakitanda Mana kalikuwa Kama vile vi double decker vya shule nikajituliza kwanza mapigo ya moyo nikawaza je ningepelekana ile laki na nusu ingekuwaje 

Akili ilichoka nikaamua niende kibandani kwa Babo

” Yani nimekuona kuanzia kule ukija unatembea Kama umelazimishwa vile unaumwa”

” Bora hata ningeumwa”

” Ila “

” Nyumba imebomoka na kugwanyika Kati kwa Kati”

” Usiniambie Hari”

” Ndo hivyo nishakiambia”

” Daa Sasa inakuwaje na hela ya mbao na bati umetoa?”

” Nako majanga Yani usingenishauri suala la genge sijui tungeishije”

” Kwanini”

” Niliyempa hela katoroka”

” Haa aisea pole”

” Pole na wewe hela si za kwetu wote”

” Sio pole ya pesa pole ya nyumba Mana kuanza upya ni mziki”

” Ndo ishatokea”

Tukakaa pale mpaka mida ya kufunga tukarudi zetu nyumbani siku ya pili nikaenda kwa bosi wangu akaniambia Harrison Leo nataka twende kule saiti nikaangalie nyumba inaendeleaje nikamwambia sawa twende akajiandaa pale tukaenda 

Tulipofika Mimi sikushuka kwenye gari nikawa nimekaa tu ndani ya gari Mara akaja Peter akagonga mlango Mana vioo vya gari vilikuwa vyeusi ilikuwa ni ngumu kumuona aliye ndani Basi nikafungua mlango wa gari

” Hari mbona uko ndani ya gari ya bosi dereva Yuko wapi?”

” Dereva ndo Mimi ndoma nipo kwenye gari”

” Acha hizo mwanangu we nimtu mzima dereva yuko wapi?”

” Peter kwani ninautani na wewe?”

” Kwahiyo umemtafuta bosi wangu mpaka ukampata ili tu ushindane na Mimi kids nilikuambia kazi hamna?”

” Peter kwasasa sihitaji malumbano na wewe bosi wako ndo bosi wangu na kila mtu anakazi yake Sasa tatizo liko wapi kuhusu kumtafuta hilo usiliwaze Sana Mana hata wewe ulimtafuta”

” Nilikuwa nakuonaga mjanja kumbe ndezi tu kwani hakuna sehemu nyingine ya kufanya kazi mpaka awe bosi wangu?”

” Sikia Peter usichukie Mimi kupata kazi kwa bosi wako Mana mshahara hulipi wewe na Wala haukatwi kwenye mshahara wako kwahiyo kila mtu afanye kazi yake “

” Unazingua wewe Ila Kama unataka tushindane poa”

” Peter mtu akipambana usiseme anasindana Mimi na shindana na shida zangu kupambana na wewe nitashindwa kufanya yangu hebu tufanye hatujawahi kuonana ili kila mtu afanye majukumu yake”

” We si mjanja poa”

Peter aliondoka ilinishangaza kumbe mtu anaweza kuchukia mafanikio ya mwingine ikiwa hata hachangii chochote nikaona potelea pote Mana muda wa ugomvi Mimi Sina Mana nishafanya ugomvi mpaka polisi walikuwa wananigwaya Ila sijaona faida yake nilichojali Mimi kwa wakati ule ni kazi 

Bosi alipomaliza tukaondoka zetu akaniambia twende kariakoo anamaduka yake kule tukaenda tukarudi jioni kabisa nikamptia Babo gengeni nikamuulizia vipi biashara akasema hivyohivyo watu bado hawajazoea Ila ni kawaida kwa unapoanza biashara unatakiwa uwavute wateja 

Maisha yalisonga Mimi nikipambana na kazi yangu na Babo akipambana na genge ulipita mwezi mwingine Babo akaniambia Harrison mtaji umezaa vipi nikurudishie ile hela Kama unamatumizi nayo au nikuze mtaji nikamwambia Mimi Sina kazi nayo kwa Sasa wewe kuza tu mtaji na ukumbuke kulipa na Kodi ya mwenye Banda akasema ameshalipa nikasema kumbe unakichwa Cha biashara akasema kwenye kutafuta hakuna kichwa unatakiwa kujiongeza tu usiseme huna kichwa nikamwambia haya pambana tukutane mwisho wa mwezi mwingine 

Kazi ikawa ni hiyo mpaka inapita miezi minne kibanda Cha Babo kimeshona akaniambia Harrison natakiwa niongeze vitu nikamuuliza Kama nini akasema mafuta ya kupikia niwe napima nikamuuliza pesa inatosha akasema ndio Basi akaongezea na mafuta pale akawa anapimia wataja wake wakija kununua mbogamboga na viungo Basi wanapata na mafuta hapohapo jina likawa kubwa na wateja kuongezeka

Sikumoja bosi wangu akaniambia Harrison kwasasa naona upumzike tu nikamuuliza kwasababu gani

Akasema ile nyumba iliyokuwa inajengwa imeisha na nimeshapata mteja atahamia siku za karibuni na kijana ambae alikuwa anasimamia ameniomba Sana awe dereva wangu kwasasa Hana kazi na siwezi kumwacha nikaona ni kijana ambe amenifanyia kazi vizuri nikashindwa kumkatalia nikamuuliza kwani Mimi katika kazi zako nimewahi kwenda tofauti? Akasema hapana Ila naomba unielewe tu Mana ni kijana wangu wa muda mrefu Sana

Nikamwambia Kama ni hivyo sawa acha Mimi nikapambane kwingine Ila nilijua tu ni figisu za Peter za kutaka kuniondoa Mana alionekana hakupendezwa na Mimi kupata kazi nikaachana nae kiroho Safi

Nikawa namsaidia Babo gengeni 

Nimwanamke ambae ni mpambanaji kweli Wala hakuwa na majivuno ni mwanamke ambae alikuwa anipa moyo wakati wote ninapokuwa Sina plani b

Basi kuna muda nilitafuta vibarua na kupata pesa kidogo nikawa naweka mwisho wa siku nikajikuta kwenye akiba Nina million moja na laki moja nikasema hii ngoja nijazie jazie nimuombe Babo ushauri tufanye nini

Siku moja Babo akaniambia Harrison nimeskia Kuna mtu amehamia siku so nyingi hapo mtaa wa pili anatafuta dereva kwanini usiende kuongea nae nikamwambia acha kesho niulizie anakaa wapi

Wakati tunaongea simu yangu ikaita Mana nilishasajili laini kwakutumia leseni yangu

Niliangalia aliyenipigia alikuwa ni bosi nikasema vipitena kunanini mpaka kanipigia simu nikapokea

” Shkamoo mzee”

” Marahaba kijana hebu naomba kesho asubuhi uje nyumbani”

Tukutane sehemu ya 15 






viuhapa

Viuhapa – habari tanzania kwa kiswahili

soma habari mbalimbali za tanzania na ulimwenguni kote kwa kiswahili hapa swahili Viu Hapa. Visit Swahili Viuhapa soma magazeti, habari za mastaa na udaku, umbea, mziki na hadithi za chombezo.

Viuhapa – Latest News and Gossip Leaks Celeb

The latest entertainment news and celeb leak staff worldwide can be found on Viu Hapa. Visit Viuhapa today for latest showbiz and celebrity.

Jobo escort – pata wadada wanaojiuza kutoka tanzania

Pata wadada wanaojiuza kutoka karibu yako hapa tanzania. wanatoa huduma zote. wapigie uongee nao..tembelea jobo escort tanzania. Malaya warembo wamejaa. Visit joboescort today for latest showbiz and celebrity.

vesgeta – Pata website kwa bei nafuu kwa ajili ya Kampuni au biashara yako.

Vesgeta Tech ni watengenezaji wa website / tovuti tanzania. wanatengeneza website kwa bei nafuu zaidi…. Visit vesgeta WATENGENEZA WEBSITE TANZANIA KWA BEI NAFUU.

https://www.swahili.viuhapa.com/mrembo-kutoka-jalalani-11-15-swahili-viuhapa/
Post a Comment

Post a Comment