AMWAIKILISHA

MAJALIWA AMWAIKILISHA RAIS SAMIA MKUTANO WA 31 WA WAKUU WA NCHI WANACHAMA WA APRM - Swahili Viuhapa

featured image





viuhapa

 

WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania itaendelea kutoa mchango wake kwenye Mpango
wa Nchi za Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) ili kuziwezesha nchi
wanachama kujifunza kwake na yenyewe iweze kujifunza kutoka kwao.

 

“Tutaendelea
kuungana na nchi wanachama kwenye mpango huu wa APRM ili tuweze kuwa sehemu ya
mchango wa maendeleo ya nchi nyingine na sisi pia tuweze kujifunza kupitia nchi
hizo katika maeneo ya kuimarisha demokrasia na utawala bora, usimamizi wa
uchumi na maendeleo ya jamii.”

 

Waziri Mkuu ameyasema
hayo leo (Ijumaa, Februari 4, 2022) alipomwakilisha Rais Samia Suluhu
Hassan katika mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali ambao ni wanachama wa APRM
uliofanyika kwa njia ya video kutokea ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma.
Mkutano huo uliongozwa Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa.

 

Amesema kuwa mpango huo pia una utaratibu wa kufanya
tafiti kwenye nchi wanachama kwa kushirikiana na taasisi za nchi husika kuona
masuala mbalimbali ya kimaendeleo, changamoto na namna ya kuzikabili changamoto
hizo.

 

Amesema kuwa mpango huo pia unatoa mafunzo kwa jamii
kupitia makundi mbalimbali ikiwemo vijana, wabunge, asasi za kiraia, wanawake
na watu wenye ulemavu na makundi mengine yanayoshiriki katika masuala ya
demokrasia na utawala bora na sekta ya uchumi. “Tutaendelea kutoa mchango wa umoja
wa Afrika na kuelezea mafanikio yetu na changamoto zetu katika umoja huo.”

 

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa kupitia mpango huo, nchi
wanachama zitaweza kupata mafanikio katika sekta mbalimbali ikiwemo uwekezaji,
ujenzi wa viwanda, kuongeza upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda,
maliasili, uvuvi na madini. “Haya yote yanaangaliwa namna ambavyo nchi inaweza
kujipanga katika kuinua uchumi wake.”

 

Amesema
kuwa Tanzania iko katika hatua za mwisho za maandalizi ya ripoti ya pili ambayo
itawasilishwa kwenye kikao kijacho cha Wakuu wa Nchi wanachama wa APRM. “Tanzania
tunatarajia kupeleka taarifa kwa mara ya pili baada ya kupata tathmini ya nchi
zote wanachama na sisi Tanzania kuona mafanikio tuliyoyapata na changamoto
tulizozipitia.”

 

Katika
mkutano huo ambao nchi za Namibia, Nigeria na Afrika Kusini ziliwasilisha
ripoti za thamini za utendaji katika maeneo mahsusi kama lilivyo lengo la APRM,
Burundi ilipokelewa kama mwanachama mpya na kufikisha nchi 42 zilizojiunga na
mpango huo.

 

Katika
mkutano huo, Rais Muhamad Buhari wa Nigeria amepitishwa kuwa mwenyekiti mpya wa
APRM akichukua nafasi ya Rais Ramaphosa.

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipomwakilisha Rais Samia
Suluhu Hassan  katika Mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali
Wanachama  wa APRM kwa njia ya Mtandao akiwa ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma, Februari 4, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)








viuhapa

Viuhapa – habari tanzania kwa kiswahili

soma habari mbalimbali za tanzania na ulimwenguni kote kwa kiswahili hapa swahili Viu Hapa. Visit Swahili Viuhapa soma magazeti, habari za mastaa na udaku, umbea, mziki na hadithi za chombezo.

Viuhapa – Latest News and Gossip Leaks Celeb

The latest entertainment news and celeb leak staff worldwide can be found on Viu Hapa. Visit Viuhapa today for latest showbiz and celebrity.

Jobo escort – pata wadada wanaojiuza kutoka tanzania

Pata wadada wanaojiuza kutoka karibu yako hapa tanzania. wanatoa huduma zote. wapigie uongee nao..tembelea jobo escort tanzania. Malaya warembo wamejaa. Visit joboescort today for latest showbiz and celebrity.

vesgeta – Pata website kwa bei nafuu kwa ajili ya Kampuni au biashara yako.

Vesgeta Tech ni watengenezaji wa website / tovuti tanzania. wanatengeneza website kwa bei nafuu zaidi…. Visit vesgeta WATENGENEZA WEBSITE TANZANIA KWA BEI NAFUU.

https://www.swahili.viuhapa.com/majaliwa-amwaikilisha-rais-samia-mkutano-wa-31-wa-wakuu-wa-nchi-wanachama-wa-aprm-swahili-viuhapa/
Post a Comment

Post a Comment