DKT

DKT. GWAJIMA: MAPAMBANO YA UKEKETAJI KWA WANAWAKE NA WATOTO NI KWA WADAU WOTE - Swahili Viuhapa

featured image





viuhapa

 

Waziri wa
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima
akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dodoma kuhusu Maadhimisho ya Siku ya
Kupinga Ukeketaji inayoadhimishwa kila tarehe 06 ya mwezi Februari.

Waziri wa
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima
akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dodoma kuhusu Maadhimisho ya Siku ya
Kupinga Ukeketaji inayoadhimishwa kila tarehe 06 ya mwezi Februari.

 

Na MJJWM- DODOMA

 

Waziri wa Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amesema vita
dhidi ya  ukatili ukiwemo Ukeketaji nchini, inatakiwa kuhusisha watu wa
kada zote ili muleta mafanikio yaliyokusudiwa.

 

Waziri Dkt. Gwajima,
ameyasema hayo jijini Dodoma, wakati akizungumza na wandishi wa Habari
ikiwa ni kuelekea kilele cha Siku ya kupinga Ukeketaji inayoadhimishwa katika
ngazi ya mikoa hasa yenye viwango vya Juu vya  Ukeketaji.

 

 Kaulimbiu ya
Siku ya Kupinga Ukeketaji kwa mwaka 2022  ni “Tuongeze Uwekezaji,
Kutokomeza Ukeketaji” ambayo inahimiza nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ikiwa
pamoja na Tanzania kuongeza uwekezaji wa rasilimali za kutosha ili kutekeleza
afua za kuzuia na kukabiliana na athari za ukeketaji ikiwa pamoja na kuwabaini
na kuwasaidia wahanga wa ukeketaji katika jamii.

 

“Hali ya ukeketaji
imekuwa inapungua mwaka hadi mwaka kunatokana na jitihada za Serikali, asasi za
kiraia na wadau wengine wanaoshiriki katika kutokomeza ukeketaji na kubadili
mitizamo ya jamii kuhusu mwanamke na mtoto wa kike”, alisema Waziri Dkt.
Gwajima. 

 

Dkt. Gwajima ameongeza
kuwa hali ya ukeketaji imepungua kutoka asilimia 18 mwaka 1996 kufikia asilimia
15 mwaka 2010 na asilimia 10 mwaka 2015/16, aidha kupungua huku bado jitihada
zaidi zinahitajika hususan kwa  Mikoa yenye hali ya juu ambayo ni 
Manyara  yenye asilimia 58, Dodoma asilimia 47, Arusha asilimia 41, 
Mara wenye asilimia 32 pamoja na Singida ambayo ina asilimia 31. 

 

Waziri Gwajima,
ameitaka jamii ikiwepo kundi la wanahabari kupaza sauti zao  kwa pamoja
katika vita hiyo, kwakutumia vyombo vyao vya Habari bila yakupotosha
kwakushirikiana na jamii na kuibua changamoto zilizopo na kuja na majibu ya
pamoja yatakayo inusuru jamii na madhila ya uekeketaji.

 

“Wadau wote
wakiwepo wanahabari tuweke mikakati ya pamoja ya kuifikia na kuelimisha jamii
katika kufikia malengo yakupunguza kutoka asilimia 8 iliyopo kwasasa hadi
asilimia 5” alisema Waziri Dkt. Gwajima

 

Dkt. Gwajima amesema,
Serikali katika kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto nchini  kwa
kushirikiana na wadau wamefanikiwa kuanzishwa kwa Kamati za Ulinzi wa Wanawake
na Watoto 18,618 kwenye Mikoa, Halmashauri, Kata hadi ngazi za Vijiji/Mtaa
mbalimbali. 

 

 

Aidha, nyumba salama 9
zimeanzishwa kwa ajili ya kuwahifadhi na kuwatunza waathirika waliokimbia
ukeketaji kwenye mikoa yenye kiwango cha juu cha ukeketaji, jitihada zingine ni
kuanzishwa kwa vituo vya mkono kwa mkono 14 kwenye Mikoa 10 ya Tanzania Bara,
sambamba na kuanzishwa kwa Dawati la Jinsia na Watoto katika vituo 420 vya
Jeshi la Polisi nchini.

 

Waziri Dkt. Gwajima,
amefafanua kuwa Serikali pia imetunga na kuzifanyia maboresho Sheria mbalimbali
ili kuimarisha ulinzi wa wanawake na watoto nchini kutokana na vitendo vya
ukatili ikiwemo Ukeketaji

 

“Sheria hizo ni pamoja
na Sheria ya Kanuni za Adhabu Sura ya 16 ya mwaka 2002, kifungu cha 158 (1) (a)
na Sheria ya Mtoto namba 21 ya mwaka 2009 ambayo inazuia ukeketaji kwa mtoto wa
kike. Aidha,  Serikali imeandaa na inatekeleza Mkakati wa Taifa wa
Kutokomeza Ukeketaji wa 2021/22 – 2024/25” amefafanua Waziri Dkt. Gwajima.








viuhapa

Viuhapa – habari tanzania kwa kiswahili

soma habari mbalimbali za tanzania na ulimwenguni kote kwa kiswahili hapa swahili Viu Hapa. Visit Swahili Viuhapa soma magazeti, habari za mastaa na udaku, umbea, mziki na hadithi za chombezo.

Viuhapa – Latest News and Gossip Leaks Celeb

The latest entertainment news and celeb leak staff worldwide can be found on Viu Hapa. Visit Viuhapa today for latest showbiz and celebrity.

Jobo escort – pata wadada wanaojiuza kutoka tanzania

Pata wadada wanaojiuza kutoka karibu yako hapa tanzania. wanatoa huduma zote. wapigie uongee nao..tembelea jobo escort tanzania. Malaya warembo wamejaa. Visit joboescort today for latest showbiz and celebrity.

vesgeta – Pata website kwa bei nafuu kwa ajili ya Kampuni au biashara yako.

Vesgeta Tech ni watengenezaji wa website / tovuti tanzania. wanatengeneza website kwa bei nafuu zaidi…. Visit vesgeta WATENGENEZA WEBSITE TANZANIA KWA BEI NAFUU.

https://www.swahili.viuhapa.com/dkt-gwajima-mapambano-ya-ukeketaji-kwa-wanawake-na-watoto-ni-kwa-wadau-wote-swahili-viuhapa/
Post a Comment

Post a Comment