Atengua

Dk Mwinyi atengua uteuzi wa viongozi watano - Swahili Viuhapa

featured image


viuhapa

 

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ametengua uteuzi wa viongozi katika Wizara za elimu, Uchumi na Uwekezaji na wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Taarifa iliyotolewa na kusainiwa na Katibu Mkuu Mtendaji, Zena Said leo Februari 3, 2022 imewataja waliotenguliwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Utumishi na Uendeshaji Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Omar Ali Omar.

Mwingine aliyetajwa katika taarifa hiyo ni Suleiman Yahya Ame Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu katika wizara hiyo ya elimu.

Wengine ni Fatma Iddi Ali, Kamishna wa Kazi katika ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji na Salum Ubwa Nassor, Ofisa Mdhamini, Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo, Pemba.

Katika orodha hiyo pia kuna Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia na Watoto katika Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Nasima Haji Choum

Ametengua nafasi hizo kuanzia leo.

logoblog


viuhapa

Viuhapa – Latest News and Gossip Leaks Celeb

The latest entertainment news and celeb leak staff worldwide can be found on Viu Hapa. Visit Viuhapa today for latest showbiz and celebrity.

https://www.swahili.viuhapa.com/dk-mwinyi-atengua-uteuzi-wa-viongozi-watano-swahili-viuhapa-2/
Post a Comment

Post a Comment