kenyanews

Uchaguzi Kenya : Matokeo ya urais yasubiriwa


MOJA KWA MOJA
Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kenya (IEBC) inatarajia kupokea fomu zote za matokeo kutoka vituo vya kupigia kura kufikia leo saa sita mchana. Tangazo la mshindi wa urais linatarajiwa kutolewa baada ya tume hiyo kuhakiki fomu hizo.

Muhtasari

IEBC inatarajia kupokea fomu zote za matokeo kutoka vituo vya kupigia kura kufikia leo saa sita mchana.

Upinzani umedai Raila Odinga alishinda uchaguzi na kuitaka tume imtangaze kuwa mshindi wa urais
Matokeo ya awali yanaonesha Bw Kenyatta anaongoza akiwa na kura 8 163 572 naye Bw Odinga ana kura 6 747 099.

Matokeo ya awali ambayo yamepokelewa ni kutoka asilimia 99.04 ya vituo.

Kura zilizoharibika zimeendelea kuwa nyingi, na kufikia sasa ni kura 399 935.


Ni maeneo bunge 20 pekee hayajawasilisha matokeo

Tume ya uchaguzi imetangaza kwamba kufikia sasa imepokea fomu za matokeo ya jumla kutoka maeneo bunge 270 kati ya 290 kote nchini humo.

Tume hiyo ilisema jana jioni kwamba inatarajia kupata Fomu 34B za matokeo kutoka maeneo yote kufikia saa sita mchana.
Post a Comment

Post a Comment