celebafrica

Wizkid apata shavu kutoka kwa rapper Future





Milango ya neema inazidi kufunguka kwa Wizkid. Msanii huyo kutoka Nigeria amepata shavu la kuwa miongoni mwa wasanii watakao tumbuiza kwenye show za ziara ya rapper Future ‘The Future Hndrxx Tour’ kutoka Marekani.

Katika ziara hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kuwaka moto Julai 8 ya mwaka huu, Wiz anatumbuiza katika show nne. Show ambazo Wizkid atawasha moto ni pamoja na itakayo fanyika West Palm Beach, Atlantic City, Syracuse na Uncasville (zote za nchini Marekani).

Kupitia mtandao wa Instagram, Wiz amethibitisha hilo kwa kuweka cover ya show zake atakazofanya na kuandika, “Catch me on the road with @future !! Bringing that African wave! 🚀🚀🚀 #starboyworldwide #freebandz.”

Ziara hiyo ya Future itazunguka karibia nchi kibao duniani ikiwemo kwenye bara la Marekani, Ulaya, Afrika na mengine. Ratiba hiyo pia imeonyesha rapper huyo wa Marekani atatumbuiza katika jijini. Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Leaders Julai 22.
Post a Comment

Post a Comment