MKONGWE wa filamu ambaye ameelekezea maisha yake kusaidia jamii, Tonto Dikeh amefanikiwa kuokoa maisha ya kijana mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja baada ya kumgonga kwa bahati mbaya.
Tukio hilo lilitokea juzi kati saa 7:40 mchana pande za Abuja ambapo Tonto alikuwa ametoka kumchukua mtoto wake katika Shule ya King Andre.
Tonto anaeleza kuwa, akiwa njiani ndani ya gari ghafla alimuona kijana huyo akikimbiza baiskeli ya matairi matatu maarufu kama Keke Napep na baada ya muda ilimshinda na kuingia katika barabara na kumgonga kisha kupoteza fahamu.
“Nilishtuka sana, mwanangu aliogopa. Nilisimamisha gari na kushuka kisha nikaanza kusimamisha magari mengine kuomba msaada. Wengi walimuangalia na kusema kuwa hatapona lakini niliamini kwa Mungu hakuna linaloshindikana.
“Hakuwa akihema wala kusema chochote, kuna waliosema angefariki muda huohuo lakini baada ya kufikishwa hospitali amepona na sasa anasaidiwa na kituo changu cha Tonto Dikeh Foundation,” alisema Tonto.[preview##eye##]
[preview##download##]