sports

Real Madrid na Atletico vitani hii leo


Hatua ya nusu fainali ya kwanza katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya (UEFA), inatarajiwa kuanza kuchezwa usiku wa leo (Jumanne). Mchezo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi duniani ni ule wa Real Madrid watakao wakaribisha Atletico Madrid katika uwanja wao wa nyumbani Santiago Bernabeu.

Hii ni mara ya tano kwa timu hizi kukutana katika michuano ya kombe hili, ambapo mara ya mwisho walikutana misimu miwili iliyopita katika hatua ya fainali ambapo Real walinyakua kombe hilo kwa jumla ya penalty 5-3, baada ya kutoka sare ya 1-1 katika dakika 120.

Mechi nyingine ya nusu fainali ya kombe hilo itawakutanisha FC Monaco dhidi ya Juventus Jumatono katika uwanja wa Stade Lois II uliopo mjini Monaco.

Mechi nyingine za marudiano zinatarajiwa kuchezwa Mei 9 na 10 ya wiki ijayo.