latest news

UJENZI WA KANISA WAENDELEA BAADA YA KUZUIWA NA MAHAKAMA JIJINI TANGA.....Bongo Hot

Viongozi na Waumini wa Kanisa la Jesus Salvation la jijini Tanga Wamejitokeza na  kufanya usafi kwenye kiwanja namba 730 kilichopo eneo la Sahare jiji hapa ikiwa nimoja ya mandalizi ya kuendeleza ujenzi wa Kanisa hilo baada ya kusimama kwa muda kutokana na Mvutano baina yao na Uwongozi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga.

Akizungumza na waandishi wa habari  wakiwa katika eneo hilo, Askofu Mama Regina  Akaro amesema kuwa kwamuda mwingi wamekuwa wanashindwa kuendelea na ujenzi kutokana na agizo kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa jiji ambalo linasema eneo hilo ni sehemu ya wazi hivyo kuacha kuendeleza ujenzi kwenye kiwanja hicho richa ya kushinda kesi zaidi ya mara moja huku Mahakama ikiamuru ujenzi wa Nyumba hiyo ya ibada uwendelezwe kwenye kiwanja chenye namba 730  ambacho kinamruhusu kuendelea na ujenzi wa kanisa lake kama ambavyo ameomba kibali hicho.

Na: Kileo kudra

Post a Comment

Post a Comment