kenya

MWANAHABARI WA KENYA AKUBALI KUKAA UTUPU SIKU YA JUMAPILI


Mwanamitindo maarufu na mwanahabari Carol Odera ni mtu wa kuvutia kutokana na matamshi yake ya ya ukakamavu.

Odera, aliyekuwa mhariri wa Drum Magazine na mwanajopo katika kipindi cha Citizen TV cha Fashion Watch amekiri kwamba si mtu wa kidini na kwa hivyo anapendelea kukaa nyumbani akiwa uchi.

"Mimi hutumia siku zangu za Jumapili nikiwa uchi kwenye sofa, pazia zikiwa zimefungwa huku nikitazama TV, na kula pop corns na mara kwa mara mimi huagizia chakula. Kama mama yumo mjini tutakula pamoja kama familia,,” alinukuliwa akisema .

Kando na kutazama TV, Odera anasema yeye hufanya yoga, kusoma na kutafakari katika siku za Jumapili.
                                          


TOA MAONI YAKO HAPA BONGOHOT