matukio

Saidi Ally amepata Mwangaza mpya baada ya Msanii Diamondplatnumz Na Mhe Makonda kumpatia msaada huu

Mungu ni mwema wakati wote.Leo kupitia kipindi cha leotena Cloudsfm bwana Said Ally au Baba D amepata mwangaza mpya katika maisha yake baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda kumpatia Msaada wa fedha shilingi Milioni 10 ambazo zitawea kumsaidi katikabiashara yake a Salon,Vilevile Mhe Makonda amemuahidi bwana Saidi kumpatia pikipiki 5 pamoja na bajaji 2 pamoja na kumnunulia nyumba ambayo itakuwa ipo katika maeneo ya karibu na mji.

Niliahidi kumsaidia Saidi baada ya ripoti ya madaktari kuonyesha kuwa hatoweza kuona tena na hivyo nikaahidi kumtafutia macho ya bandia,kumpatia millioni 10 fimbo a kutembelea na darasa la kijifunzia la watu wasioona,Lakini pia nawashukuru sana Watanzania wanaotoa Michango,Lakini pia nimefanya jitihada kuongea na wadau mbalimbali nimefanikiwa kupata bodaboda 5,bajaji 2 na nyumba> Mhe Makonda

Vilevile Msanii Diamond Platumz ambaye ameguswa na swala hilo la bwana saidi amejitokeza hapo hapo katika kipindi cha leoetena na kumkabidhi Saidi shilingi milioni mbili.



Kufika kwangu hapa ni kumwambia Saidi kila jambo hupangwa na Mwenyezi Mungu huenda amekuepusha mambo mengi zaidi mbele> DiamondDiamond

Kwa yoyote ambaye atakuwa na chochote cha kuweza kumuongezea bwana Said Ally unaweza kumfikishia mchango wako kupitia CRDB akaunti namba 0152226886400 au unaweza kumtumia kupitia namba yake 0714 200255
Share this:
Post a Comment

Post a Comment