fashion

WASHIRIKI WA MISS TANGA WATABIRI MISS TANZANIA KUTOKA TANGA....(PICHA)


Itakapotimia Tarehe July 30 2016 Asubuhi Katika jiji la Tanga watakuwa tayari wameshapata mwakilishi atakayeshiriki miss Tanzania


Washiriki wa Umiss katika mkoa wa Tanga wamekuwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika mashindano hayo. Baada ya kutembelewa hapo jana na majaji wa shindano hilo litakalofanyika siku ya Ijumaa ya July 29.

Muandaaji wa shindano hilo kupitia wilaya ya Temeke Ndugu Bernad Kisaka ambaye pia ni Jaji wa shindano hilo kwa mkoa wa Tanga amezungumza jana na washiriki hao na kuwapa nafasi ya kuuliza vitu mbalimbali.

Washiriki walipata nafasi hiyo ya kipekee na kuonyesha ujasiri wao katika shindano hilo licha ya kuwa pia ni warembo wenye vigezo vyote vya kushiriki shindano hilo na kupata mshiriki atakayenyakua Taji la miss Tanzania akitokea mkoa wa Tanga.

Waandaaji wa shindano hilo la umiss kwa Tanzania ni Lino International Agency, Katika mkoa wa Tanga waandaaji wa shindano hilo ni Kituo cha Redio TANGA KUNANI (TK FM) iliyopo mkoani hapo tanga wakiwa sambamba na website yako ya BONGOHOTZ.COM

Tazama picha...

Mwandishi wa Habari akitoa mchango wa maneno kwa washiriki
Jaji wa miss Tanga akiongea na washiriki. wa pembeni kushoto ni Said Othman mmiliki wa TK fm

Mamiss wakisikiliza kwa umakini
Ndugu.Said akiongea na mamiss




Baadhi ya watangazaji wa TK FM

Post a Comment

Post a Comment