BAADA ya tetesi kuzagaa kuwa ni wapenzi wa ‘kupika na kupakua’ hatimaye staa wa Hip Hop Bongo, Bilnas ameweka wazi uhusiano wake na msanii mwenzake, Estelina Sanga ‘Linah kuwa si wapenzi bali ni marafiki walioshibana tu.
Bilnas anayebamba na Ngoma ya Chafu Pozi alienda mbali zaidi na kusema kuwa, ameanza kumjua Linah kutokana na kuwa na ukaribu na Zuwena Mohammed ‘Shilole’.linah
“Nakumbuka nilikuwa na shoo Zanzibar ambapo ilitakiwa tuwe na Shilole pamoja na Linah, sasa kwa kuwa nilikuwa karibu na Shilole hapo ndipo nikamfahamu Linah na kuanzia hapo tukawa marafiki wa kusapotiana kwenye muziki na si vinginevyo,” alisema Bilnas.