sports

Mchezaji wa Chelsea Didier Drogba Achukua Maamuzi Magumu Kuhusu Kuendelea Kuichezea Chelsea..Soma Hapa







Ligi kuu ya Uingereza leo inafikia ukingoni, huku klabu ya Chelsea wakiwa ndio mabingwa wa ligi hiyo.
Siku ya leo itakuwa ina mchanganyiko wa furaha na huzuni kwa mashabiki wakereketwa wa Chelsea, kwa sababu watakuwa wanakabidhiwa kombe lao rasmi lakini pia itakuwa ndio mwisho wao kumuona gwiji wa klabu hiyo Didier Drogba akiwa anaichezea timu hiyo.
Kupitia akaunti yak rasmi ya mtandao wa kijamii wa Instagram – Drogba ametangaza kwamba leo ndio itakuwa siku yake ya mwisho kuitumikia Chelsea dimbani



Drogba anasema amezungumza na Kocha Jose Mourinho kuhusu hatma yake na amemuelewa kwamba angependa kuendelea kucheza soka japo kwa msimu mmoja. Hivyo ili aendelee kupata nafasi ya kucheza anahitaji kwenda sehemu nyingine.
Drogba amewatakia kila kheri mashabiki wa  Chelsea na ameahidi kurudi kufanya kazi na klabu hiyo huko mbeleni.





















Post a Comment

Post a Comment