tanzia

BAD NEWS: PAPA WEMBA AFARIKI DUNIA AKIWA JUKWAANI...



TANZIA: Taarifa za awali kutoka kituo cha Utangazaji cha France 24 zinasema kwamba Papa Wemba amefariki muda mfupi baada ya kuanguka ghalfa akiwa anatumbuiza wimbo wa tatu jukwaani akiwa na Magic System na kupoteza fahamu, kwenye tamasha aliloalikwa kutumbuiza.

 Mwanamuziki nguli wa Bolingo kutoka Demokrasia ya Congo, Jules Shughu Wembadio Pene Kikumba maarufu kwa jina la Papa Wemba amefariki dunia huko Abidjan, Ivory Coast akiwa jukwaani.

Taarifa za awali kutoka kituo cha Utangazaji cha France 24 zinasema kwamba Papa Wemba amefariki muda mfupi baada ya kuanguka ghalfa akiwa anatumbuiza wimbo wa tatu jukwaani akiwa na Magic System na kupoteza fahamu, kwenye tamasha aliloalikwa kutumbuiza.

Redio ya Kongo, Radio Okapi imetangaza taarifa za kifo chake kwamba kimetokea nchini humo alikokwenda kutumbuiza kwenye tamasha la muziki la Anoumabo (FEMUA)

Kutoka katika mitandao mbalimbali ya kuaminika duniani, imeelezwa kuwa Papa Wemba aliyefariki akiwa na umri wa miaka 66, alidondoka wiki moja iliyopita na kulazwa hospitalini akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) kwa takribani wiki moja kabla ya kufariki usiku wa kuamkia leo.

Chanzo cha kifo cha mkongwe huyo katika muziki wa dansi duniani bado hakijajulikana.


Jiunge na BONGOHOTZ.COM sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usiache ku download application play store kupata habari ndani ya sekunde kila inapotufikia..Karibu

LIKE PAGE YA BONGOHOTZ KWENYE FACEBOOK



TOA MAONI YAKO HAPA

Post a Comment

Post a Comment