gossip

GIGY MONEY AJIREKODI VIDEO YA UTUPU



Video Queen anayezitendea haki video za wasanii mbalimbali hapa Bongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’ ameambulia matusi na maneno ya dhihaka kutoka kwa mashabiki wake mbalimbali baada ya juzikati kutupia video ya utupu katika akaunti yake katika Mtandao wa Kijamii wa Instagram.
gigy

Wakionesha kukerwa na kitendo hicho, mashabiki hao walionekana kuchukizwa na kitendo hicho hivyo kumjia juu mrembo huyo ambaye ameuza nyago katika video mbalimbali ikiwemo ya Shika Adabu Yako ya Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.

Mara baada ya kuyasoma matusi hayo, Gigy aliamua kuitoa video hiyo haraka kwani kadiri muda ulivyozidi kwenda mbele, ndivyo watu walivyozidi kumtukana, hali iliyoonekana kumvuruga.

“Huyu dada ni jipu na anahitaji kutumbuliwa. Haiwezekani afanye vitu kama hivi. Hii si video ya kuweka katika mtandao wa kijamii ambayo inafunguliwa hadi na watoto. Angalia hata picha zake nyingine zimejaa utata, nadhani TCRA inatakiwa kumtumbua japo kidogo,” alisema mdau mmoja mara baada ya kuiona video hiyo na picha kibao za mrembo huyo.

Mara baada ya kuinyaka video hiyo kwa ‘kui-screenshot’, gazeti hili lilijaribu kumtafuta Gigy ili aizungumzie video hiyo na kutoa sababu ya kuiweka lakini hakupokea simu.

Chanzo:GPL

 Share
Post a Comment

Post a Comment