job vacancy

JOB VACANCY: Ajira Katika Sekretarieti Ya Utumishi wa Umma


TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
 Kumb. Na EA.7/96/01/H/90 20 Novemba, 2015
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 400 za kazi kama zilivyoorodheshwa katika tangazo hili.

1.0
 MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA II – NAFASI 25

1.1
 MAJUKUMU YA KAZI

 Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi
  • Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi

 kusimamia uwindaji wa kitalii na utalii wa picha

 kulinda Nyara za Serikali

 Kusimamia usafirishaji wa wanyamapori na nyara nje na ndani ya Nchi

 Kusimamia matumizi ya magari ya doria

 Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya wanyamapori na kutunza takwimu zao

 Kuratibu uingiaji wa wageni katika Mapori ya Akiba

 Kudhibiti moto katika hifadhi

 Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa ushahidi Mahakamani

 Kukusanya takwimu za wanyama na mimea kwenye hifadhi

Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na taaluma yake

1.2
 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au kidato cha VI wenye Stashahada ya Uhifadhi Wanyamapori (Diploma in Wildlife Management) kutoka Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Mweka au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

1.3
 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.

2.0
 MSAIDIZI WA HESABU (ACCOUNTS ASSISTANT) - NAFASI 10

2.1
 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuandika na kutunza “register” zinazohusu shughuli za uhasibu.

 Kuandika hati za malipo na hati za mapokezi ya fedha.

 Kutunza majalada yenye kumbukumbu za hesabu

 Kupeleka barua/nyaraka za uhasibu Benki.

 Kufanya usuluhisho wa masurufu, karadha, Hesabu za Benki na Amana.

2.2
 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Cheti cha ATEC level II au “Foundation Level” kinachotolewa na NBAA

2.3
 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B kwa mwezi

3.1
 AFISA MICHEZO DARAJA LA II (GAMES AND SPORTS OFFICER GRADE II) – NAFASI 15

3.1
 MAJUKUMU YA KAZI
 Kufundisha fani mbalimbali kwa Waalimu wa vyuo, shule, na vituo vya Elimu na Mafunzo

 Kufundisha fani mbalimbali za michezo kwa waalimu, Makocha, viongozi wa vyama na vilabu vya michezo

 Kufundisha fani mbalimbali za michezo kwa Timu za Michezo mbalimbali.

3.2
 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa mwenye Shahada au Stashahada ya Juu ya Elimu ya Michezo (Physical Education) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

3.3
 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi.

4.1
 WAKILI WA SERIKALI DARAJA LA II - (NAFASI 7)

4.1
 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuendesha mashauri mepesi  Mahakamani

 Kuendesha kesi  za mahakama kuu

 Kutoa Ushauri wa Kisheria kwa Serikali chini ya usimamiziwa Mawakili Waandamizi

 Kushughulikia kesi za vizazi, vifo, ndoa, na kesi zinazotokana na mirathi mahakamani.

 Kusimamia utayarishaji wa takwimu zinazohusu ndoa, talaka, mabadiliko na mabatilisho ya ndoa..

 Kutayarisha maandishi juu ya Sheria ambazo Serikali/Tume ya kurekebisha Sheria inataka zifanyiwe utafiti na kurekebishwa.

 Kufanya utafiti wa Sheria.

 Kuelimisha Umma kuhusu mambo ya Katiba na Haki za Binadamu.

4.2
 SIFA ZA MWOMBAJI
 Mwenye Shahada ya Sheria (LLB) Kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali na Serikali na kumaliza vizuri mafunzo katika kazi (Internship) ya mwaka mmoja katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

4.3
 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia mishahara ya Serikali yaani TGS E

5.1
 KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III – NAFASI 50

5.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.

 Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.

 Kusaidia kutunza taarifa / kumbukumbu zamatukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba na kazi zingine. Zilizo pangwa kutekelezwa katika ofisi anamo fanyia kazi, na kumuarifu Mkuu wake kwawakati unao hitajika.

 Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinacho hitajika katikashughulizakazihapoofisini.

 Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.

 Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazo husika.

 Kutekeleza kazi zozote atakazo kuwa amepangiwa na Msimamizi wake wakazi.

5.2
 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wakidato cha IV waliohudhuria Mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa Hatua ya Tatu. Wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na kiingereza maneno 80 kwadakika moja na wawe wamepata mafunzo ya kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika program za Windows, Microsoft Office, Internet, E-mail na Publisher.

5.3
 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi

6.1
 AFISA WA SHERIA DARAJA LA II (LEGAL OFFICER GRADE II) – NAFASI 30

6.1
 MAJUKUMU YA KAZI
Hili ni daraja la mafunzo katika kazi, hivyo Maafisa wa Sheria katika daraja hili watafanya kazi za kisheria kwa maelekezo ya Maafisa wa Sheria Waandamizi ikiwa ni pamoja na:

 Kutoa ushauri na kufanya utafiti wa kisheria pale anapohitajika kulingana na Wizara, Idara ya Serikali ama sehemu aliko.

 Kufanya mawasiliano na ofisi nyingine kuhusu masuala ya kisheria kwa maelekezo ya Maafisa wa Sheria walio katika ngazi za juu.

6.2
 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza ya Sheria kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na waliomaliza mafunzo ya uwakili yanayotambuliwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

6.3
 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi

7.0
 FUNDI SANIFU DARAJA LA II - UMEME (TECHNICIAN GRADE II ELECTRICAL) – NAFASI 25

7.1
 MAJUKUMU YA KAZI
 Kufanya ukaguzi wa ubora wa magari ya Serikali na kurekebisha ipasavyo.

 Kufanya upimaji wa Mitambo na Umeme kufuatana na Maelekezo ya Mhandisi.

 Kufanya kazi za kutengeneza  mitambo, magari,na vifaa vya Umeme

 Kufanya usanifu wa miradi midogo midogo ya umeme

 Kusimamia jinsi ya kufunga mashine mpya zinazowekwa kwenye karakana za ufundi na Umeme.

7.2
 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye mojawapo ya sifa zilizotajwa hapa chini:

 Waliohitimu kidato cha VI na kufuzu mafunzo ya ufundi ya miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali katika moja ya fani za ufundi.

 Waliohitimu kidato cha IV na kufuzu kozi ya ufundi ya miaka mitatu kutoka Vyuo vya Ufundi vinavyotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani za ufundi,

 Wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi hatua ya I kutoka Chuo cha Ufundi kinachotambuliwa na Serikali,

 Wenye Stashahada ya Kawaida katika fani za ufundi kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

7.3
 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi

8.0
 AFISA UFUGAJI NYUKI DARAJA LA II (BEEKEEPING OFFICER GRADE II) – NAFASI 20

8.1
 MAJUKUMU YA KAZI

 Kusimamia uanzishaji wa hifadhi za nyuki na manzuki.

 Kutangaza Sera na Sheria za ufugaji nyuki.

 Kufundisha masomo ya fani ya ufugaji nyuki.

 Kukusanya takwimu za rasilimali na ufugaji nyuki.

 Kupanga na kupima ubora wa mazao ya nyuki.

8.2
 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wenye Shahada katika fani ya Ufugaji Nyuki au Sayansi ya Elimu ya Mimea, Elimu ya Wadudu au Elimu ya Wanyama kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

8.3
 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.

9.1
 MTUNZA BUSTANI DARAJA LA II - (GARDNER II) NAFASI 3

9.2
 MAJUKUMU YA KAZI
 Kupanda mboga, matunda, n.k. katika bustani.

 Kupalilia mazao katika bustani.

 Kupanda maua katika maeneo yanayohusika.

 Kupanda na kukata majani na kumwagilia maji.

 Kufanya kazi zingine zitakazoelekezwa na Viongozi wa Kitengo chao.

9.2
 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa  wenye  Cheti  katika  fani  ya  utunzaji  bustani  za  maua,  mboga  na

upandaji majani kutoka chuo cha Maendeleo ya Wananchi, VETA, au JKT au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali wenye uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka mitatu.

9.3
 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS.A  kwa mwezi.

10.0
 MWANDAZI DARAJA LA II (WAITER GRADE II) - NAFASI 1

10.1
 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuandaa meza ya kulia chakula.

 Kupamba meza ya kulia chakula

 Kupanga vifaa vya kulia chakula mezani.

 Kuondoa vyombo baada ya kula chakula

10.2
 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wenye cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV na kufuzu mafunzo si chini ya mwaka mmoja katika fani ya ‘Food and Bevarages’ yatolewayo na vyuo vya

Forodhani Dar es Salaam. Masoka Moshi, Arusha Hotel na Y.M.C.A ya Moshi na Vyuo vingine vinavyolingana ambavyo vitatambuliwa na Serikali.

10.3
 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.B kwa mwezi.

11.0
 DOBI DARAJA LA II – NAFASI 1

11.1
 MAJUKUMU YA KAZI
 Kufanya uchambuzi wa nguo kwa ajili ya kuosha, kukausha, kunyoosha na kuzifungasha.

11.2
 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofuzu mafunzo ya miaka miwili au
 mitatu   katika   fani   ya   Dobi   (Laundry   Services)   kutoka   katika   vyuo
 vinavyotambuliwa na Serikali.
11.3
 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS. C kwa mwezi.

12.1
 MPISHI DARAJA LA II (COOK II ) NAFASI - 5

12.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuandaa chakula cha wanachuo kulingana na Menyu na idadi ya wanachuo

 Kupika chakula cha wanachuo

 Kutoa ushauri kwa uongozi wa chuo kuhusu chakula cha wanachuo.

 Kusimamia jiko.

12.2
 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne/sita waliofuzu mafunzo ya cheti yasiyopungua mwaka mmoja katika fani ya food Production kutoka vyuo vinavyotambuliwa na serikali.

12.3
 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi

13.1
 MKUTUBI DARAJA LA II – NAFASI 1

13.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuratibu shughuli za ukuzaji wa utamaduni kitaifa.

 Kuratibu na kusimamia shughuli za ukaguzi na udhibiti maonyesho ya filamu na video katika ngazi ya taifa.

 Kushauri juu ya mitaala ya mafunzo na elimu ya fani za utamaduni.

 Kusimamia usajili wa vikundi na vyama vya fani za utamaduni.

 Kushauri juu ya ujenzi wa majukwaa na majumba ya utamaduni yenye hadhi ya kitaifa.

 Kuratibu shughuli za utafiti wa mila na desturi nchini.

 Kusimamia na kuratibu ukuzaji wa matumizi fasaha na sanifu ya Kiswahili nchini.

 Kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa kituo.

13.2
 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza katika fani ya ukutubi au sifa inayolingana
 na hiyo kutoka katika vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.
13.3
 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.

14.1
 AFISA LISHE II (NUTRITON OFFICEER II) – NAFASI 4

14.1
 MAJUKUMU YA KAZI

 Kukusanya taarifa na takwimu za lishe kutoka kwa wadau na makundi mbalimbali na kutoa ushauri kuhusu lishe bora katika ngazi ya wilaya.

 Kuchambua takwimu za lishe na kuandaa taarifa ya watoto na makundi mengine yenye lishe duni.

 Kushiriki katika kuandaa mipango na bajeti ya lishe katika ngazi ya wialaya.

 Kutoa taarifa za mara kwa mara za hali ya lishe katika ngazi ya wilaya.

 Kusimamia kazi za lishe katika wilaya

 Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.

14.2
 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajriwa wenye Shahada ya kwanza ya Lishe, Sayansi Kimu na Lishe au Sayansi na Chakula na Teknolojia ya Chakula (BSc – Nutrition, Home Economics and Nutrition, Food Science and Technology Food Science) au Stashahada ya juu ya Lishe (Higher Diploma in Nutrition) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

14.3
 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi.

15.0
 AFISA ARDHI MSAIDIZI – NAFASI 1

15.1  MAJUKUMU YA KAZI
 Kuingiza kumbukumbu katika kompyuta

 Kutoa ushauri kwa wateja.

 Kupokea, kukagua na kusambaza majalada kwa maafisa kwa utekelezaji.

 Kusaidia Maafisa Ardhi katika ukaguzi na kuchukua kumbukumbu, picha taarifa, vipimo vya majumba na michoro.

 Kujumuisha na kuandaa taarifa za ukaguzi.

 Kuandaa rasimu za Hati na uingizaji wa plani ya Hati (deed plan)

 Kuagiza plani za Hati (Deed Plan)

15.2
 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne au Kidato cha Sita, waliofuzu mafunzo ya
 miaka miwili ya Umiliki Ardhi na Uthamini kutoka Vyuo vya Ardhi au Vyuo Vikuu
 vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
15.3
 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C

16.0
 DEREVA DARAJA LA II (DRIVER II) – NAFASI 178

16.1
 MAJUKUMU YA KAZI

 Kuendesha magari ya abiria, magari madogo na malori

 Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote, na kufanya uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo,

 Kufanya matengenezo madogo madogo katika gari,

 Kutunza na kuandika daftari la safari “Log-book” kwa safari zote.

16.2
 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV, Wenye Leseni daraja la “C” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha ajali na wenye Cheti cha Majaribio ya ufundi Daraja la II.

16.3
 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.

17.0
 MPOKEZI (RECEPTIONIST) – NAFASI 1

17.1
 MAJUKUMU YA KAZI
 Kupokea wageni na kuwasaili shida zao.

 Kutunza rejesta ya wageni wa ofisi na kufanya uchambuzi wa wageni wanaoingia ili kutoa ushauri juu ya utaratibu bora wa kupokea wageni.

 Kupokea na kusambaza maombi ya simu za ndani.

 Kutunza na kudumisha usafi wa “Switchboard” na ofisi zake.

 Kuwaelekeza wageni wa ofisi kwa maafisa/ofisi watakakopewa huduma.

 Kuhakikisha kwamba wageni wanaoingia ndani wanamiadi (Appointment) au wamepata idhni ya maafisa husika.

 Kupokea simu kutoka nje na kuzisambaza kwa maofisa mbalimbali ofisini.

 Kupokea simu kutoka “Extension” za ndani na kupiga nje ya ofisi.

 Kutunza rejesta ya simu zinazopokelewa kutoka nje ya ofisi na zinazopigwa kwenda nje.


17.2
 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV waliofaulu masomo ya Kiingereza, Kiswahili na Hisabati na kufuzu mafunzo ya Mapokezi na Upokeaji Simu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

17.3
 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi

18.1
 AFISA USAFIRISHAJI DARAJA LA II (TRANSPORT OFFICER GRADE II ) –

NAFASI 1

18.1
 MAJUKUMU YA KAZI

 Kutayarisha gharama za uendeshaji wa usafiri kwa ajili ya kusaidia kutoa maamuzi.

 Kuhakikisha kuwa takwimu na kumbukumbu zinazohusu vyombo vya usafiri pamoja na mitandao yake zinatunzwa vyema na kwa usahihi. Kuandaa takwimu zinazohusu maendeleo ya ukuaji wa sekta ya usafirishaji, na kuwasilisha kwa watumiaji ndani na nje ya nchi.

 Kukusanya takwimu za usafirishaji nchini.

 Kukadiria na kushauri juu ya utendaji wa miradi mbalimnbali ya sekta ya usafirishaji.

 Kutekeleza majukumu mengine yanayohusu sekta ya usafirishaji

18.2
 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada Juu ya kawaida ya Usafirishaji kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

19.1
 MHANDISI DARAJA LA II - MAJI (WATER ENGINEER GRADE II) – (NAFASI 10)

19.1
 MAJUKUMU YA KAZI

 Ujenzi na Usimamizi wa Vituo vya Hali ya Hewa, Vituo vya Upimaji wingi wa Maji mitoni (Discharge Measurements) na Uchukuaji wa sampuli za mchanga unaosafirishwa kwenye mito (sedment sampling) na kuzitafsiri.

 Ukusanyaji wa takwimu kwenye vituo vya hali ya hewa na upimaji wa wingi wa maji mitoni na kuzitafsri takwimu hizo.

 Kuandaa na kutayarisha Taarifa ya robo, nusu na mwaka mzima katika sehemu ya Haidrologia.

 Kutayarisha kielelezo cha mtiririko wa maji ( Rating Curve Eqution )

19.2
 SIFA ZA MWOMBAJI


 Kuajiriwa mwenye Shahada ya Uhandisi wa Rasilimali za Maji kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali. Wawe na ujuzi wa kutumia kompyuta.

19.3
 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.

20.0
 AFISA UTAMADUNI MSAIDIZI (ASSISTANT CULTURAL OFFICER GRADE) – NAFASI- 2

20.1
 MAJUKUMU YA KAZI

 Kufundisha fani mbalimbali za utamaduni katika Vyuo na Vituo vya Elimu na mafunzo ya utamaduni.

20.2
 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wenye stashahada ya kawaida kutoka chuo cha Sanaa Bagamoyo au chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

20.3
 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C Kwa mwezi.

21.1
 BARAZA LA KISWAHILI LA TAIFA (BAKITA)

Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) liliundwa kwa sheria ya Bunge Na. 27 ya mwaka 1967 na kufanyiwa marekebisho mwaka 1983. Kutokana na sheria hii Baraza ndilo mratibu wa kusimamia asasi na mawakala wote wanaokuza Kiswahili katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

21.1
 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU I-  NAFASI 1
21.2
 MAJUKUMU YA KAZI

 Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajiwa na wasomaji.

 Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka.

 Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makundi kulingana na somo husika (classification and boxing) kwa ajili ya matumizi ya ofisi.

 Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki (file racks/cabinets) katika masjala/vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu.

 Kuweka na kumbukumbu (barua, nyaraka nk) katika mafaili.

 Kushughulikia maombi ya kumbukumbu/nyaraka kutoka Taasisi za Serikali.

 Kupokea na kusambaza nyaraka.

 Kufanya kazi zingine kama atakavyoagizwa na msimamizi wake wa kazi.

21.3
 SIFA ZA MWOMBAJI

 Stashahada katika fani ya masjala kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

 Uwezo wa kutumia kompyuta.

 Uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka mitatu katika fani ya utunzaji kumbukumbu.

22.1
 MSAIDIZI MIFUGO (LIVESTOCK FIELD ASSISTANTS) – NAFASI 3

22.1
 MAJUKUMU YA KAZI

 Kutoa huduma za ugani katika uendelezaji mifugo na mazao yake,

 Kutibu mifugo na kutoa taarifa za magonjwa, tiba na chakula,

 Kusimamia utendaji kazi wa wahudumu mifugo,

 Kutunza takwimu na taarifa mbalimbali za mifugo,

 Kukaguo ubora wa mazao ya mifugo,

 Kusimamia ustawi wa wanyama,

 Kufanya kaza nyingine atakazo pangiwa na msimamizi wake wa kazi zinazohusiana na fani yake.

22.2
 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV ambao wamepata mafunzo ya mifugo ya muda wa miaka miwili na kutunukiwa Astashahada (certificate) ya uzalishaji na afya ya mifugo kutoka vyuo vya mafunzo ya mifugo. (Livestock Training Institute

– LITI) au chuo chochote kinachotambuliwa na serikali.

22.3
 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B Kwa mwezi.

23.0
 MSAIDIZI WA MAKTABA (LIBRARY ASSISTANT) - NAFASI 3

23.1
 MAJUKUMU YA KAZI

 Kuandikisha wasomaji.

 Kupanga vitabu katika rafu (Shelves)

 Kuazimisha na kupokea vitabu vinavyoazimwa.

 Kukarabati vitabu vilivyochakaa,

 Kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wa kituo.

23.2
 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa waliohitimu cheti cha Mtihani wa Taifa wa kidato cha IV ambao wamefaulu mafunzo ya Wasaidizi wa Maktaba (National Library Assistants Certificate Course) yatolewayo na Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania au wenye cheti kinacholingana na hicho.

23.3
 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS. B kwa mwezi.

24.0
 MHANDISI RADIO (RADIO ENGINEER) II – 1 NAFASI

24.1
 MAJUKUMU YA KAZI

 Uendeshaji wa mitambo ya Radio chini ya usimamizi wa wahandisi wazoefu.

 Matengenezo madogo madogo ya mitambo ya Radio.

 Anaweza kuteuliwa kuwa kiongozi wa zamu “Shift Leader”.

 Kuchunguza, kuchambua na kurekebisha mitambo ya Radio

 Kusimamia na kuongoza Mafundi Mitambo walio chini yake.

24.2
 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wenye Shahada ya Juu ya Uhandisi kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani za Uhandisi.

24.3
 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS. E kwa mwezi.

25.0
 BARAZA LA SANAA LA TAIFA (BASATA)

Baraza la Sanaa la Taifa ni shirika la Umma lililoundwa kwa sheria ya Bunge Na. 23 ya mwaka 1984. (Sheria ya kuunda upya Baraza la Sanaa la Taifa kwa kuunganisha Baraza la Sanaa la Taifa na Baraza la Muziki la Taifa na kufuta Sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa ya mwaka 1974 na Sheria ya Baraza la Muziki la Taifa ya mwaka 1974 na kuweka utaratibu kuhusiana na mambo hayo.

Kazi za Baraza la Sanaa la Taifa ni Kufufua, kukuza na kuendeleza kazi za sanaa ikiwa nI pamoja na Uhamasishaji, Usimamizi, Uimarishaji, Uratibu, Utafiti, na Ushauri wa kazi mbalimbali za Sanaa.

25.1
 MKURUGENZI WA UTAFITI NA UKUZAJI WA STADI ZA WASANII

25.2
 MAJUKUMU YA KAZI

 Kuongoza Idara ya Utafiti na ukuzaji wa stadi za Sanaa.

 Kuandaa mpango wa Utafiti na kusimamia utekelezaji.

 Kuandaa mpango wa kukuza stadi za wasanii na kusimamia utekelezaji.

 Kuwasiliana na watafiti mbali mbali na kushirikiana nao.

 Kuandaa na kusimamia makubaliano na watafiti wanaojiajiri kwa muda kufanya tafiti maalum

 Kubaini na kuteua wawezeshaji wa ukuzaji wa stadi za wasanii.

 Kusimamia uchapishaji wa majarida na vitabu vya Baraza.

25.3
 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wenye Shahada ya Uzamili katika fani za Sanaa na Utafiti kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na serikali.

 Uzoefu wa kazi usiopungua miaka 8 Miaka 5 kati ya hiyo ikiwa ni katika nafasi ya uongozi wa idara mbalimbali zilizo chini ya taasisi za umma.

25.4
 MSHAHARA

 Mshahara PGSS 14

25.5
 MPOKEZI – 1 NAFASI

25.6
 MAJUKUMU YA KAZI

 Kupokea wageni na kuwaelekeza sehemu na maafisa kuonana nao.

 Kupokea barua zinazoletwa kwa mkono.

 Kushauri wageni juu ya mamlaka sahihi ya kushughulikia kero au shida zao.

 Kufanya kazi nyingine atakazoagizwa na mkuu wake.

25.7
 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wenye Elimu ya kidato cha nne Elimu ya kidato cha nne na cheti cha kompyuta.

25.8
 MSHAHARA

 Mshahara PGSS 2.

NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.

i.
 Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45

ii.
 Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.

iii.
 Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao ili wajiridhishe ipasavyo.

iv.
 Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza ( Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)

watatu wa kuaminika.

v.
 Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.

-
 Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.

-
 Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI

-
 Computer Certificate

-
 Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)

-
 Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.

vi.
 Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)

HAVITAKUBALIWA.

vii.
 Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).

viii.
 Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

ix.
 Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.

x.
 Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

xi.
 Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 4 Desemba, 2015

xii.
 Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira HAURUHUSIWI.

xiii.
 Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kingereza.

xiv.
 Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;

 http://portal.ajira.go.tz/

(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)

xv.
 MUHIMU: KUMBUKA KUWEKA (ATTACH) BARUA YAKO YA MAOMBI. ANUANI YA BARUA HIYO IELEKEZWE KWA KATIBU, OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA S.L.P 63100 DAR ES SALAAM
Post a Comment

Post a Comment