international

WIZKID AELEZEA KIUNDANI ZAIDI KUHUSU KUSUSIA NA BET AWARDS



Staa wa Nigeria, Wizkid ambaye alikuwa akiwania kipengele cha Best International Act:Africa katika BET Awards 2015, ni msanii wa pili aliyesusia tuzo hizo zilizotolewa Jumalipi iliyopita huko L.A, Marekani.

Baada ya Fuse ODG kutweet akisema sababu zilizomfanya asihudhurie utolewaji wa tuzo hizo, Wizkid naye amesema hatakuwa akihudhuria pre-shows na nominee parties kama utaratibu wa kuwapa tuzo wasanii wa Africa mapema kabla ya show yenyewe (saa 4 asubuhi) backstage utaendelea.

Alianza kwa kutweet:

Lol, nasikia BET wamemaind kwa sababu sikuhudhuria pre-shows na Interviews! LOl


Wizkid ameongeza kuwa utaratibu wa kuwabagua wasanii wa Afrika katika tuzo hizo ndio ilikuwa sababu ya kutohudhuria hata aliposhinda tuzo ya BET kwa mara ya kwanza.

Ameongeza kuwa hiyo ndio sababu kubwa pia ya kutopost kitu katika mitandao ya kijamii kuhusu nominations au tuzo hizo kwa ujumla sababu yeye hajali.


Hizi ndio tweet zake




 
Post a Comment

Post a Comment