TECHNOLOGY
AZAM TV wafungua studio ya kisasa yenye thamani ya sh bilioni 53....IONE ILIVYO HAPA
0
Comments
Leo ni uzinduzi wa studio mpya za Azam zilizopo Tabata Dar es Salaam, wazo ambalo lilitolewa March 8, 2014 na tenda hio kupewa kampuni kutoka Uingereza na kuigharimu Azam zaidi ya bilioni 53. Kulingana na maelezo ya Tido ndio studio bora zaidi Tanzania mpaka sasa. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Jakaya Kikwete. Kuna wageni wengi waalikwa wakiwemo James Mbatia, Mwigulu Nchemba, Prof Lipumba, Filbert Bayi, Jamal Malinzi, Taji Liundi na wengineo.
Mwigulu: Mmeonyesha uzalendo katika matangazo, mwekezaji aliewekaza katika studio hii ameonekana kuwa na mafanikio kila anapowekeza kwenye sekta nyingine, tupo kwenye safari kuifanya nchi kuwa ya kiwango cha kati, tunahitaji serious investors ambao ni watanzania na wataajiri wafanyakazi wa kiwango cha kati.
Mbatia: Kazi kubwa ya vyombo vya habari kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha, vyombo kama hivi vinafikisha taarifa mapema
Prof J (Mwanamuziki): Azam anazidi kuvuka mipaka na kuuza kazi zetu nje, tuendelee kuwapa sapoti.
Mpinga: Itasaidia katika kuelimisha, kwa upande wangu naomba pia wajikite katika kuelimisha mambo ya barabarani
Post a Comment