sports

Serengeti Boys yafuzu AFCON U-17 Baada ya kushinda Rufaa


Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, ‘Serengeti Boys’ hatimaye imefuzu kushiriki fainali za Afrika zitakazofanyika nchini Gabon, Aprili mwaka huu.

Serengeti imefuzu baada ya kushinda rufaa waliiyomkatia mchezaji wa Congo Brazzaville, Langa-Lesse Bercy anayedaiwa kuwa na umri mkubwa aliyetakiwa kwenda kupimwa vipimo maalum cha kuthibitisha umri halisi.

Taarifa zilizopatikana jana Ijumaa jioni kutoka mkutano wa CAF nchini Gabon zilidai Serengeti ilipewa nafasi hiyo na sasa itakuwa kati ya timu 8 zitakazocheza fainali hizo.

Waziri wa Michezo, Nape Nnauye ameipongeza timu hiyo katika ujumbe wake kupitia akaunti yake ya Twitter.

“Mungu Mkubwa! Tumefuzu kwenda fainali za Afrika Chini ya Umri wa miaka 17. NIA, UWEZO NA SABABU ZA KUCHUKUA KOMBE HILI TUNAZO. HONGERA TZ!,” alitweet waziri huyo.



TOA MAONI YAKO HAPA BONGOHOT